Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Friday, 17 June 2016

Kutoka Bungeni June 16, 2016: Idadi ya Wabunge Waliosimamishwa Kuhudhuria Vikao vya Bunge Yaongezeka..

Kamati ya bunge imejadili na kuamua kuwasimamisha wabunge wawili wa Chadema baada ya kutoa taarifa za uongo ndani ya bunge, wabunge hao ni pamoja na Susan Lymo na Anatropia Theonest.
Katika bunge hilo lilofanyika June 16, Mbunge Susan Lymo ambae amesimamisa vikao kuanzia June 17 hadi 24, alilidanganya bunge baada ya kusema kuwa Jeshi la Polisi Limenunua Magari 777 ya washawasha ikiwa ni idadi ya magari ambayo yamepangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa matumizi mbalimbali.
Nae Anatropia Theonest alilidanya bunge baada ya kusema kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Hivyo kamati ya bunge kuamua kumsimamisha kutohudhuria vikao vitatu vya bunge.

Follow us on our facebook page; Kwetutz24.com and follow us on twitter: @kwetutz24 and Pininterest: @kwetutz24 

Tuesday, 14 June 2016

POLISI WOTE NCHINI KUKUMBWA NA ADHABU HII...


Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi Willium Ole Nasha amesema kuwa Serikali Imetangaza adhabu ya kuwakata mishahara na adhabu nyingine, askari Polisi wote nchini ambao hawata wapigia saluti wabunge wa Bunge la Muungano na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema haya wakati akijibu swali kutoka kwa mbunge wa viti Maalum (CCM) Fakharia Khamis, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na kuongeza kuwa Askari yoyote ambae hatotoa saluti ataripotiwa kwa kiongozi wake ambapo atapewa adhabu ikiwemo kukatwa mshahara, kupigishwa paredi na adhabu nyinginezo.
Naibu huyo pia alisema kuwa sheria hiyo imetajwa kwa vyeo vyote kuwa wanatakiwa kupiga saluti kwa Rais wa Bara na Zanzibar, kwa makamu wote  wa Rais wa Zanzibar  na wengineyo kama Spika.

Tuesday, 10 May 2016

Nauli za Mabasi yaendayo Kasi Zatangazwa....

Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na majini Sumatra imetangazi nauli mpya zitakazotumika kwa Mabasi yaendayo haraka jiijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Sumatra Gillard Ngewe amesema kuwa mradi huo ambao umekwishaanza siku ya leo utasafirisha watu bure jumanne ambayo ni leo na Jumatano, mradi huo utakuwa na nauli zifuatazo; sh. 400, 650 na 800. huku wanafunzi wakilipa Sh.200 tu bila kujali umbali.

Tuesday, 15 March 2016

Vigogo watatu Rahco Wafikishwa Kortini

Mkurugenzi Mkuu wa zamanni wa Kampuni ya Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania RAHCO Benardhard Tito pamoja na wenzake wawili, wamefikishwa kortini katika Mahakama Kuu ya Kisutu Mkazi jijini Dar es Salaam,  wakikabiliwa na mashtaka manne.

Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka haya, Matumizi mabaya ya madaraka, Kuhujumu uchumi, Kula njama na kusababishia serikali hasara ya dola za Marekani 527, 540.
Washatakiwa wawili ni mfanyabiashara na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild Property Limited(SouthAfrika)  anayedaiwa kuwa dalali wa zabuni, Kanji Mwinyijuma na aliyekuwa Katibu na mwanansheria  wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe.
Washitakiwa hao watatu walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba huku pembeni akiwemo wakili Mkuu wa serikali, Timon Vitalis, Maghela Ndimbo na Janeth Machulya kutoka Takukuru.
Mashtaka hayo yakiongozwa na Wakili Vitalis Timon, washtakiwa wote watatu kwa nyakati tofauti kati ya September mosi 2014 na September 30, 2015 mkoa wa Dar es Salaam, washtakiwa hawa watatu walikula njama   ya kutenda makosa hayo chini ya Sheria ya Kuzia na Kupambana na Rushwa.
Katika Kesi hiyo, Februari 27, 2015 Tito mwaka jana katika ofisi za kampuini hiyo zilizopo Ilala Dar es Salaam, alitumia vibaya madaraka baada ya kuidhinisha kampuni ya Rothschild (South Africa) Property kuwa mshauri katika mpango wa ujenzi wa Reli ya Kati, bila kuidhinishwa na Bodi ya Zabuni ya Kampuni hiyo.
Machi 12, 2014 katika ofisi za Rahco, Tito na Massawe wanadaiwa kuwa walisaini barua ya kuikubali kampuni ya Rothschild (South Africa) Property kutoa huduma ya ushauri wa kifedha katika ujenzi wa Reli ya Kati bila kuidhinishwa na bodi.
Aidha, Kati ya Machi 12 na Mei 20, 2015 wanadaiwa kuwa, wakiwa ofisini kwao, waliacha majukumu yao kwa kushindwa kuwasilisha mkataba wa Kampuni ya Rothschild kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
kati ya Mei 20 na Juni 20, 2015, walishindwa kuwasilisha nakala za mkataba wa makubaliano wa kampuni hiyo na kampuni ya Rahco, kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkaguzi wa ndani na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Pia washitakiwa hao kwa nyakati tofauti, kati ya Machi Mosi na Septemba 30, mwaka jana washitakiw wote watatu kwa pamoja walikubaliana kuidhinisha makubaliano ya kampuni hiyo katika masuala ya kiushauri na kusababishia kampuni hasara ya dola za Kimarekani 527, 540, ambazo zilishalipwa kiwango cha awali benki.
Agosti 18, 2015, Tito alitelekeza majukumu yake na alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa zabuni ya upendeleo kwa kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China Construction Corporation. Inadaiwa katika zabuni hiyo, kampuni ilipewe kazi ya ujenzi wa reli ya kilometa mbili yenye kiwango cha kisasa kuanzia Soga ikiwa na thamani ya dola za Marekani 2, 312, 229.39 bila kuidhinishwa na Bodi ya Zabuni ya Rahco.
Washitakiwa wote watatu hawakuruhusiwa kujibu mashtaka hayo kwakuwa Mhakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu. Uamuzi wa dhamana utatolewa siku ya Ijumaa.

Monday, 14 March 2016

Kesi ya Wenje Kusimamisha Shughuli Mwanza.


Shughuli mbalimbali za kijamii katikati ya jiji la Mwanza zimesimama kwa zaidi ya saa moja,wakati mamia ya wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ) walipokuwa wakitoka mahakama kuu kanda ya Mwanza kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Nyamagana iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje.
Wafuasi hao wa CHADEMA walifunga mitaa yote ya jiji la Mwanza, majira ya saa sita mchana wakati wakitoka Mahakamani kusikiliza kesi ya uchaguzi namba 3 ya Mwaka 2016, iliyofunguliwa na Ezekiel Wenje dhidi ya mbunge wa sasa wa jimbo la Nyamagana Mh.Stanslaus Mabula hatua iliyosababisha baadhi ya maduka kufungwa na usafiri wa daladala kusimama kwa muda kwa hofu ya kuibuka vurugu.
ITV imeshuhudia Defender za polisi zikiwa na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ( FFU ),wenye silaha za moto na mabomu ya machozi zikifanya doria katika mitaa ya katikati ya jiji pamoja na viunga vya mahakama kuu, ambako tangu asubuhi mamia ya wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh. Freeman Mbowe walikuwa wamepiga kambi kwa ajili ya kufuatilia kesi hiyo inayosikilizwa na jaji kakusulo sambo.
 
Wafuasi hao wa CHADEMA ambao walitoka Mahakamani hapo wakikimbia huku wakiimba na kushangilia kuelekea Hoteli ya Gold Crest,baadhi yao walijikuta wakiwa mikononi mwa Polisi na wengine kupata Mkong’oto na kuswekwa rumande kwa kushindwa kutii amri halali ya polisi iliyowataka kuwa watulivu,jambo ambalo limelalamikiwa na baadhi ya wafuasi hao katika mahojiano na ITV.
 
Katika hatua nyingine jaji wa mahakama ya rufaa Mh.Rosemary Ibrahim ametupilia mbali kwa gharama maombi ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa oktoba 25 Mwaka jana, yaliyokatiwa rufaa na wapiga kura wanne wa jimbo la bunda mjini dhidi ya mbunge wa jimbo hilo Mh. Esther Bulaya,kufuatia makosa ya kisheria yaliyojitokeza kwenye kiapo kilichoapwa na mtu mwingine na kuthibitishwa na mtu mwingine.
 
Jaji Ibrahimu amesema Mahakama hiyo imeamua kutoa uamuzi huo kulingana na sheria zinavyoelekeza baada ya wakili wa wapeleka maombi Costantine Mutalemwa na Denis Kahangwa kukiri kuwapo kwa kosa hilo na kutoa mifano ya kesi zilizowahi kuamriwa na mahakama nyingine kwa kuonyesha hazikuwa na makosa kama hayo bali aliyeapa kiapo hicho ndiye aliyethibitisha ila kulikuwa na makosa madogomadogo yaliyokubalika kufanyiwa marekebisho tofauti na hilo.
Taarifa >>>>>ITV
 

Tuesday, 16 February 2016

Vigogo Wanne wa Bodi ya Mikopo Wasimamishwa Kazi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Prof. Joice Ndalichako amemsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya mikopo wa elimu ya juu (HESLB) George Nyatenga kutokana na utendaji wake wa kazi usioridhisha.
waliotajwa wengine bkufutwa kazi ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo, Juma Chagonja pamoja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo, Onesmo Laizer.
Tazama video hapa chini.

Tuesday, 19 January 2016

Gazeti la Mawio lafutwa kwenye orordha ya magazeti Nchini.

Waziri wa Habari, michezo, sanaa na utamaduni Nape Nnauye amelifungia rasmi gazeti maarufu hapa nchini Mawio ikiwa pamoja na kufungia shughuli zote za usambazaji na uchapishaji wa gazeti hilo. Moaja ya sabau alizo toa waziri huyo juu ya kulifuta gazeti hilo kwenye orodha ya magazeti hapa nchini ni kuwa wahariri wa gazeti hilo wamekuwa na kiburi mbele ya serikali pale wanapoambiwa wajitetee kuhusu habari wanazo ziandika.
Akizungumza na waandhishi wa habari siku hiyo, Nape alisema kuwa sharia ya magazeti ya mwaka 1976 sura ya 229 kifungu cha 25 kinampa mamlaka ya kulifungia gazeti hilo, na kwanzia  terehe 15 January mwaka huu amelifuta gazeti hilo kwenye orodha ya msajili ikiwa pamoja na kulipiga marufuku kuchapisha kwenye mitandao .
 Waziri aliendelea kwa kutaja sababu ya serikali kufikia hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo, ni baada ya ofisi ya msajili wa magazeti kuwaandikia barua wahariri wa gazeti hilo,kwa kuwataka wasahihishe makosa yao tangu 2013 jambo analodai kuwa wahariri wake wamekuwa wakiijibu majibu mabaya serikali.
"Yaani wahariri wa hili gazeti tangu mwaka 2013 tunawaambia wabadilishe aina ya uandishi wa habari lakini wakawa wanaijibu serikali majibu mabaya na wakawa wanaendelea kuandika habari ya uchochezi na kuharibu amani ya nchi,”
Pamoja na hayo Waziri amevitaka vyombo vya habari pamoja na wahariri kuzingstia sharia na kanunu za taratibu za nchi kwa kuandika habari zenye kufuata weledi.
Baada ya tukio hilo. Wahariri wa Gazeti la Mawio Saimon Mkina na Jabir Idrissa  walisakwa na jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam, ambapo walivamia ofisi mbili za gazeti hilo kwa kosa la kuandika kwenye gazeti hilo toleo 152 ya Alhamisi ya tarehe 13 January mwaka huu,japo kuwa waliwakosa.

Kichwa cha Habari cha Gazeti hilo kilisema, "Machafuko Yaja Zanzibar.

Aidha mmoja wa wamiliki wa gazeti hilo ambae hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa amezipokea taarifa za kufungiwa kwa gazeti hilo, ila wako mbioni kulifufua gazeti lilokufa, iliwaewndelee na kazi zilizokuwa zikifanywa na gazeti lilofungwa.











Thursday, 31 December 2015

Kamanda Suleiman Kova Astaafu Rasmi

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam Suleiman Kova amestaafu rasmi hivi leo Dec. 31, 2015 baada yakulitumikia ueshi hilo kwa mda mrefu sasa.

Akizungumza na watanzania hivi leo asubuhi kupitia kipindi cha Kumakucha cha ITV, amesema kuwa mkataba wake na jeshi la polisi nchin umekwisha hivyo analaimika kukaa pembeni na kumwachia majukumu hayo mtu mwingine.
Mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi”, alisema Kamanda Kova.
Kamanda Kova alikuwa Kamanda w Kanda Maalum Dar es Salaam na kwa mujibu wake ameweza kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa tangu aianza kazi yake.

Tuesday, 29 December 2015

Zanzibar: CUF yashutumu wito wa CCM



Taarifa kutoka>>>>>BBC SWAHILI
Chama cha CUF visiwani Zanzibar kimewataka wananchi visiwani humo kupuuza wito wa chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuwataka wazanzibari wajiandae kwa marudio ya uchaguzi visiwani humo.



Mwandishi wa BBC Sammy Awami anasema kuwa CUF anasema kwamba wito wa CCM juu ya maandalizi ya uchaguzi wakati bado vikao vya usuruhishi wa mgogoro huo bado vinaendelea, ni kuwachanganya wananchi juu ya nini hasa hatma ya mgogoro wa kisiasa visiwani humo
Kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja sasa, viongozi wa juu wa serikali na vyama, ikiwa ni pamoja na marais wastaafu wamekuwa wakiendelea na vikao vya siri vinavyolenga kutafuta suluhu la mgogoro huo wa kisiasa visiwani Zanzibar
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Kaimu mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa CUF Ismail Jussa amesema
''ni vema ikasubiriwa taarifa rasmi ya maafikiano ya vikao vinavyoendelea ambayo bado haijatolewa''


Tangu kufutwa kwa uchaguzi visiwani Zanzibar, chama tawala CCM kiliunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi huku CUF ikiapa kuususia uchaguzi huo na kutaka aliyekuwa mgombea urais wake Maalim Seif Sharif Hamad atangazwe kuwa mshindi wa uchaguzi huo, ambao CUF inadai Maalim Seif alishinda kwa asilimia zaidi ya 50%.
Wanaohusika katika msururu wa vikao vya mashauriano ya mgogoro wa Zanzibar ni pamoja na Rais wa Zanzibar Dokta Ali Mohamed Shein, ambaye ndiye mwenyekiti huku wajumbe wakiwa ni makamu wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi, marais wastaafu Amani Abeid Karume, Jakaya Mrisho Kikwete, Ali Hassan Mwinyi, Dokta Salmin Amour Juma na makamu wa kwanza wa rais Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye ndiye mwakilishi kutoka upande wa CUF.
Zanzibar iliingia katika mgogoro wa kisiasa miezi miwili iliyopita baada ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi visiwani humo Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi kwa kile alichokiita ukiukwaji wa sheria na utaratibu wakati wa zoezi la upigaji kura.

Wednesday, 23 December 2015

Magufuli Amalizia Uteuzi wake wa Mawaziri Aliwabakiza

Rais Magufuli hivi leo amemalizia uteuzi wake wa mawaziri na manaibu wake amabo hakuwamalizia pindi alipotangaza baraza jipya la kwanza la  Mawaziri katika awamu yake ya Tano.

Uteuzi
1. Professa Jumanne Maghembe -  Waziri wa Maliasili na Utalii
2. Dkt. Philip Mpango - Waziri wa Fedha na Mipango 9ni baada ya kteuliwa kuwa Mbunge)
3. Mhandisi Gerson Lwenge - Waziri wa Maji na Umwagiliaji
4. Dkt. Joyce Naelichako - Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia, na Ufundi (ni baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge)
5, Mh. Hamad Masauni - Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
6. Prof. Makame Mbarawa - Amehamishwa kutoka Wizara ya Naji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.
Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU 23 Desemba, 2015

Tuesday, 22 December 2015

Dr.MAGUFULI AMSIMAMISHA AFISA RAHCO

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania RAHCO, Mhandisi Benhadard Tito.  baada- ya kutuhumiwa   kukiuka taratibu za manunuzi katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati..
Magufuli alichukua hatua hiyo kali baada ya mkutano na wadau wanaohusika na ujenzi wa reli ya kisasa yaani “Standard Gauge”
Uchunguzi wa kimsingi unaelekezwa kwa utoaji wa zabuni hiyo inayokisiwa kugharimu takriban dola milioni $14.

Sasa Magufuli al maarufu "The Bulldozer" ameiagiza mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.
Si hao tu walioathirika na amri hiyo ya rais Magufuli, bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) pia imevunjiliwa mbali.

jeshi La Polisi Linawashikilia Askari 6 kwa Mauaji

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia Askari sita baada ya kuua watuhumiwa wawili wa Ujangili huku mtuhumiwa mmoja akiendelea kusakwa.
Kamanda wa Kikosi Sulemani Kova amesema wawili kati ya hao sita walikuwa ni Polisi huku wane wakiwa ni Askari wa wanyama pori Kikosi Kazi Maalum cha kuzuia ujangili..
wawali hao  waliofariki walitambulika kwa majina  Moja akiwa Yasini Rashidi (46) aliyekuwa Mkazi wa Mabibo pamoja na Samson Masigara(46) aliyekuwa mkazi wa Mbezi.
"Taarifa za mwanzo  zinasema kuwa Askari hawa pamoja na mwenzao walikuwa wakiwafuatilia watu wawili kwa tuhuma za kujihusisha na  ujangili....na msako ulipangwa kufanyika Dec. 19
Uchunguzi ukabaini kuwa kulikuwa na utata tangu tuko hili linafabyika wakati wakiwasaka wawili hawa mpaka kifo ndio maana tumeamua kuwashikilia ilikupata  ukweli wa vifo hivi na uhalali wa nguvu iliyotumika.. alisema
Hata hhivto askari hao walishindwa kutoa taarifa za kutosha na ukweli kuhusu tukio hilo kwakuwa siku hiyo ya tukio kulikuwa hakuna majibizano ya risasi baina yao na watuhmiwa hao wawili wa ujangili..

Friday, 4 December 2015

Dr. Magufuli Atoa Kiama kwa Wafanyabiashara

Dr. Magufuli ametoa siku saba kwa wafanyabiashara  wote waliokwepa kulipa kodi baaada ya kupitisha makontena kinyemela kinyume na sheria,na kusema kuwa atawachukulia hatua za kisheria endapo hawatalipa kodi hizo.

Alityazungumza haya hapo jana wakati akiofanya mkutano wake wa kwanza na  wadau kutoka sekta binafsi TPSF jijini Dar Es Salaaam. Wakizungumza kuhusu sekta binafsi katika kukuza uchumi na wajibu wa serikali katika kutengeneza mazingira wezeshi
Dr. Magufuli alizitaka sekta binafsi kuongeza uwekezaji wake na kuangalia fursa nyingine ambazo ni muhimu katika kujenga nchini.
"Wale wenye makontena wasijifiche, ninatoa siku saba weakalipe kodi, tukiwakamata sheria itafuata.Nina uhakika sekta binafsi mkijipanga turtaikomboa hii nchi. Alisema Magufuli wakati akizungumza na wadau wa sekta binasfi.
Pia alitaka sekta binafsi kushirikiana na serikali ili kuboresha maisha ya wananchi.

Monday, 27 July 2015

ZITTO KABWE; ACT ITASIMAMA YENYEWE

ZITTO KABWE; ACT ITASIMAMA YENYEWE
Zitto Kabwe siku ya jana asema rasmi kwamba chama chake cha ACT kuwa kia simama chenywe katika uchaguzi mkuu 2015, na kwamba hakitajiunga na UKAWA. aliyasema haya siku ya jana akiwa anazungumza na vyombo vya habari. 

" Najua chama chetu bado kichanga kina miezi mitano tangu kuanza kwake lakini si mnaijua timu ya soka ya Mbeya city? aliuliza swali hili kwenye kikao hicho wakasema "ndiyo", ile timu ilioanza kimasiara  lakini mwishowe ikawa tishio kwa timu za ligi kuu basi chama hiki kitakuwa hivyo" alisema Zitto.
Kiongozi huyo Mkuu wa ACT alizima keleel na minong'ono iliyokuwepo miongoni mwa wanachama wake juu ya kuhamia UKAWA. alisema pia wanampango wa kuunda kampeni za kisayansi kwani hayo ni mapambano ya kufa na kupona. na hivyo hakina mpango wa kujiunga na UKAWA.