Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Friday, 17 June 2016

Kutoka Bungeni June 16, 2016: Idadi ya Wabunge Waliosimamishwa Kuhudhuria Vikao vya Bunge Yaongezeka..

Kamati ya bunge imejadili na kuamua kuwasimamisha wabunge wawili wa Chadema baada ya kutoa taarifa za uongo ndani ya bunge, wabunge hao ni pamoja na Susan Lymo na Anatropia Theonest.
Katika bunge hilo lilofanyika June 16, Mbunge Susan Lymo ambae amesimamisa vikao kuanzia June 17 hadi 24, alilidanganya bunge baada ya kusema kuwa Jeshi la Polisi Limenunua Magari 777 ya washawasha ikiwa ni idadi ya magari ambayo yamepangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa matumizi mbalimbali.
Nae Anatropia Theonest alilidanya bunge baada ya kusema kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Hivyo kamati ya bunge kuamua kumsimamisha kutohudhuria vikao vitatu vya bunge.

Follow us on our facebook page; Kwetutz24.com and follow us on twitter: @kwetutz24 and Pininterest: @kwetutz24 

Tuesday, 14 June 2016

POLISI WOTE NCHINI KUKUMBWA NA ADHABU HII...


Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi Willium Ole Nasha amesema kuwa Serikali Imetangaza adhabu ya kuwakata mishahara na adhabu nyingine, askari Polisi wote nchini ambao hawata wapigia saluti wabunge wa Bunge la Muungano na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema haya wakati akijibu swali kutoka kwa mbunge wa viti Maalum (CCM) Fakharia Khamis, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na kuongeza kuwa Askari yoyote ambae hatotoa saluti ataripotiwa kwa kiongozi wake ambapo atapewa adhabu ikiwemo kukatwa mshahara, kupigishwa paredi na adhabu nyinginezo.
Naibu huyo pia alisema kuwa sheria hiyo imetajwa kwa vyeo vyote kuwa wanatakiwa kupiga saluti kwa Rais wa Bara na Zanzibar, kwa makamu wote  wa Rais wa Zanzibar  na wengineyo kama Spika.

Tuesday, 10 May 2016

Nauli za Mabasi yaendayo Kasi Zatangazwa....

Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na majini Sumatra imetangazi nauli mpya zitakazotumika kwa Mabasi yaendayo haraka jiijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Sumatra Gillard Ngewe amesema kuwa mradi huo ambao umekwishaanza siku ya leo utasafirisha watu bure jumanne ambayo ni leo na Jumatano, mradi huo utakuwa na nauli zifuatazo; sh. 400, 650 na 800. huku wanafunzi wakilipa Sh.200 tu bila kujali umbali.

Tuesday, 15 March 2016

Vigogo watatu Rahco Wafikishwa Kortini

Mkurugenzi Mkuu wa zamanni wa Kampuni ya Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania RAHCO Benardhard Tito pamoja na wenzake wawili, wamefikishwa kortini katika Mahakama Kuu ya Kisutu Mkazi jijini Dar es Salaam,  wakikabiliwa na mashtaka manne.

Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka haya, Matumizi mabaya ya madaraka, Kuhujumu uchumi, Kula njama na kusababishia serikali hasara ya dola za Marekani 527, 540.
Washatakiwa wawili ni mfanyabiashara na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild Property Limited(SouthAfrika)  anayedaiwa kuwa dalali wa zabuni, Kanji Mwinyijuma na aliyekuwa Katibu na mwanansheria  wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe.
Washitakiwa hao watatu walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba huku pembeni akiwemo wakili Mkuu wa serikali, Timon Vitalis, Maghela Ndimbo na Janeth Machulya kutoka Takukuru.
Mashtaka hayo yakiongozwa na Wakili Vitalis Timon, washtakiwa wote watatu kwa nyakati tofauti kati ya September mosi 2014 na September 30, 2015 mkoa wa Dar es Salaam, washtakiwa hawa watatu walikula njama   ya kutenda makosa hayo chini ya Sheria ya Kuzia na Kupambana na Rushwa.
Katika Kesi hiyo, Februari 27, 2015 Tito mwaka jana katika ofisi za kampuini hiyo zilizopo Ilala Dar es Salaam, alitumia vibaya madaraka baada ya kuidhinisha kampuni ya Rothschild (South Africa) Property kuwa mshauri katika mpango wa ujenzi wa Reli ya Kati, bila kuidhinishwa na Bodi ya Zabuni ya Kampuni hiyo.
Machi 12, 2014 katika ofisi za Rahco, Tito na Massawe wanadaiwa kuwa walisaini barua ya kuikubali kampuni ya Rothschild (South Africa) Property kutoa huduma ya ushauri wa kifedha katika ujenzi wa Reli ya Kati bila kuidhinishwa na bodi.
Aidha, Kati ya Machi 12 na Mei 20, 2015 wanadaiwa kuwa, wakiwa ofisini kwao, waliacha majukumu yao kwa kushindwa kuwasilisha mkataba wa Kampuni ya Rothschild kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
kati ya Mei 20 na Juni 20, 2015, walishindwa kuwasilisha nakala za mkataba wa makubaliano wa kampuni hiyo na kampuni ya Rahco, kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkaguzi wa ndani na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Pia washitakiwa hao kwa nyakati tofauti, kati ya Machi Mosi na Septemba 30, mwaka jana washitakiw wote watatu kwa pamoja walikubaliana kuidhinisha makubaliano ya kampuni hiyo katika masuala ya kiushauri na kusababishia kampuni hasara ya dola za Kimarekani 527, 540, ambazo zilishalipwa kiwango cha awali benki.
Agosti 18, 2015, Tito alitelekeza majukumu yake na alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa zabuni ya upendeleo kwa kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China Construction Corporation. Inadaiwa katika zabuni hiyo, kampuni ilipewe kazi ya ujenzi wa reli ya kilometa mbili yenye kiwango cha kisasa kuanzia Soga ikiwa na thamani ya dola za Marekani 2, 312, 229.39 bila kuidhinishwa na Bodi ya Zabuni ya Rahco.
Washitakiwa wote watatu hawakuruhusiwa kujibu mashtaka hayo kwakuwa Mhakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu. Uamuzi wa dhamana utatolewa siku ya Ijumaa.

Monday, 14 March 2016

Kesi ya Wenje Kusimamisha Shughuli Mwanza.


Shughuli mbalimbali za kijamii katikati ya jiji la Mwanza zimesimama kwa zaidi ya saa moja,wakati mamia ya wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ) walipokuwa wakitoka mahakama kuu kanda ya Mwanza kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Nyamagana iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje.
Wafuasi hao wa CHADEMA walifunga mitaa yote ya jiji la Mwanza, majira ya saa sita mchana wakati wakitoka Mahakamani kusikiliza kesi ya uchaguzi namba 3 ya Mwaka 2016, iliyofunguliwa na Ezekiel Wenje dhidi ya mbunge wa sasa wa jimbo la Nyamagana Mh.Stanslaus Mabula hatua iliyosababisha baadhi ya maduka kufungwa na usafiri wa daladala kusimama kwa muda kwa hofu ya kuibuka vurugu.
ITV imeshuhudia Defender za polisi zikiwa na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ( FFU ),wenye silaha za moto na mabomu ya machozi zikifanya doria katika mitaa ya katikati ya jiji pamoja na viunga vya mahakama kuu, ambako tangu asubuhi mamia ya wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh. Freeman Mbowe walikuwa wamepiga kambi kwa ajili ya kufuatilia kesi hiyo inayosikilizwa na jaji kakusulo sambo.
 
Wafuasi hao wa CHADEMA ambao walitoka Mahakamani hapo wakikimbia huku wakiimba na kushangilia kuelekea Hoteli ya Gold Crest,baadhi yao walijikuta wakiwa mikononi mwa Polisi na wengine kupata Mkong’oto na kuswekwa rumande kwa kushindwa kutii amri halali ya polisi iliyowataka kuwa watulivu,jambo ambalo limelalamikiwa na baadhi ya wafuasi hao katika mahojiano na ITV.
 
Katika hatua nyingine jaji wa mahakama ya rufaa Mh.Rosemary Ibrahim ametupilia mbali kwa gharama maombi ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa oktoba 25 Mwaka jana, yaliyokatiwa rufaa na wapiga kura wanne wa jimbo la bunda mjini dhidi ya mbunge wa jimbo hilo Mh. Esther Bulaya,kufuatia makosa ya kisheria yaliyojitokeza kwenye kiapo kilichoapwa na mtu mwingine na kuthibitishwa na mtu mwingine.
 
Jaji Ibrahimu amesema Mahakama hiyo imeamua kutoa uamuzi huo kulingana na sheria zinavyoelekeza baada ya wakili wa wapeleka maombi Costantine Mutalemwa na Denis Kahangwa kukiri kuwapo kwa kosa hilo na kutoa mifano ya kesi zilizowahi kuamriwa na mahakama nyingine kwa kuonyesha hazikuwa na makosa kama hayo bali aliyeapa kiapo hicho ndiye aliyethibitisha ila kulikuwa na makosa madogomadogo yaliyokubalika kufanyiwa marekebisho tofauti na hilo.
Taarifa >>>>>ITV
 

Tuesday, 16 February 2016

Vigogo Wanne wa Bodi ya Mikopo Wasimamishwa Kazi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Prof. Joice Ndalichako amemsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya mikopo wa elimu ya juu (HESLB) George Nyatenga kutokana na utendaji wake wa kazi usioridhisha.
waliotajwa wengine bkufutwa kazi ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo, Juma Chagonja pamoja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo, Onesmo Laizer.
Tazama video hapa chini.