Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Monday, 15 August 2016

Rais wa Zambia Atangazwa Mshindi Uchaguzi Mkuu

Rais wa Zambia Edger Lungu ametangazwa mshindi wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Urais nchini humo.
Edgar Lungu alishida kwa asilimia 50.35 ya kura huku mpinzani wake Hakainde Hichilemi ambae ni mfanya biashara mkubwa nchini humo aliyeshnda kwa asilimia 47.67 kama Tume ya Uchaguzi ilivyotangaza.
Chama cha Upinzani upande wa Hichilema UNPD kilijitoa mapepma katika uhakiki wa kura zilizopigwa na raia wa nchi hiyo kwa madai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu mkubwa.
Uchaguzi mkuu wa Urais Zambia ulifanyika siku ya Alhamis wiki iliyopita.

Saturday, 16 July 2016

Maelfu ya Wanajeshi Washikiliwa Uturuki Baada ya Jaribio la Kupindua Nchi Kufeli....



Yildirim ambae ni Waziri Mkuu nchini Uturuki ameeleza kuwa tukio hilo la Mapinduzi limekuwa doa kwa Demokrasia nchini humo.
karibu Wanajeshi 2889 wanashikiliwa pamoja na Maafisa wa Ngazi za Juu baadaya mpango wa kufanya Mapinduzi nchini humo kugomga mwamba.

Jaribio hilo la Mapinduzi halikufanikiwa nchini humo alieleza Jenerali Umit Dundar huku waliopanga njama hiyo 104 wakiuwawawa kutokana tukio hilo. Huku wengine 161  ambao ni polisi pamoja na Raia wamekufa wakati wakupigania uhuru wanchi hiyo na 1440 wakielezwa kuwa na Majeraha
Milio ya risasi na milipuko ya mabomu ilisikika Usiku mima katika miji ya Ankara na Istanbul ambapo inasadikika wanajeshi Zaidi ya 1500 walikamatwa.

Saturday, 28 May 2016

Rais Wa Somalia Ataka Njia Muafaka kuwarudisha wakimbizi katika Taifa lake...


Rais wa Somalia ametaka kuwepo kwa njia muafaka ya kuwarudisha wakimbizii nchi kwake, huku Kenya ikisisitiza kuwa itaendelea na mpango wake wa kufunga kambi kubwa duniani.
Kambi ya Dadaab imekuwa kimbilio la wasomalia zaidi ya 300, 000.\
Rais Hassam Sheik Mohamed  ameiambia BBC  kuondolewa kwa lazima kwa wakimbizi hao haikuwa maslahi ya taifa lolote..
Kenya imesema inataka kufunga kambi kutokana na hali usalama, wakisema kuwa mashambulizi katika ardhi yao yamekuwa yakilengwa kwenye kambi hiyo..
Kenya haikutilia maanani vitisho vile vilivyo fanyika mwezi Aprili kufuatia mashambulizi ya vifo vya wanamgambo wa kundi la kisomali la Al- shabaab Kilomita 100 kutoka eneo la chuo..
Kundi la al-Qaeda linalohusishwa na mashambulzi hayo limekuwa likifanya mashambulio kadhaa nchini Kenya katika miaka ya hivi karibuni.
Akizungumza na BBC Rais Maohameid amesema kwamba, Uongozi unatakiwa kufanya makubaliano  katika kutafuta njia bora ya kuwarudisha watu hao katika taifa lao na katika hali inayoeleweka kulingana na sheria za kimataifa. Hatutaki mahusiano yetu yaathiriwe na Kenya,
Aliendelea kusema kuwa Kenya ilikuwa na msaada mkubwa katika kuwahifandhi wakimbizi kwa kipindi cha mda mrefu sasa na imekuwa ikijituma katika kuwarejesha watu wa taifa lake.
Daadab ilianzishwa mwaka 1991 kwa wanafamilia waliokuwa wakiikimbia Somalia kutoka na migogoro na baadhi ya watu wamekuwa wakiishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20.

Wednesday, 27 April 2016

Lucy Kibaki Afariki Akiwa London..

Aliyekuwa Mke wa kwanza wa Rais, Lucy Kibaki nchi Kenya amefariki siku ya Jumanne, April 26 akiwa London katika hospitali iliyojukikana kwa jina la Bupa Cromwell hospital iliyoko huko London akitibiwa.
Kibaki amefariki kutoka na ugonjwa usio julikana uliokuwa ukimsumbua kwa mwezi tangu alipotolewa kutoka hospiali ya Kenya siku ya Juamamosi April 23 na kuhamishiwa London kwa matibabu zaidi.
Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki, pamoja na mawe Judy na Antony walikuwa karibu yake mpaka kifo kilipomkuta.
Lucy alipata umaarufu kwa kumchapa kofi mpiga picha mmoja mwaka 2005 wakati alipovamia afisi za kituo kimoja cha habari mwaka 2005 akikasirishwa na vile habari moja ilivyoandikwa.
Lucy alizaliwa mwaka 1940, hakuweza kuoneka hadharani tena tangu mume wake Mwai Kibaki aachie Uongozi kwa Uhuru Kenyata, mara ya mwisho kuonekana ilikuwa ni 2010, wakati alipofurahishwa na kupatikana kwa katiba mpya.


Saturday, 20 February 2016

Museven Atangazwa Mshindi wa Urais Nchini Uganda

Tume ya Uchaguzi ya Nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa urais kwa muula wa tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamis ya Febr. 18, 2016.
Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu. Huku  Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye akipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Chama kikuu cha upinzani nchini humo kimeyakataa matokeo hayo wakidai kuwa ni udanganyifu.
Museveni alitangazwa mshindi wakati mpinzani wake mkuu Dkt. Kizza Besigye, akitumikia kifungo cha nyumbani chini ya ulinzi mkali wa polisi.  mjini Kampala.
Chama tawala NRM kimewaomba wagombea wote kuheshimu matakwa ya wananchin na kuwaomba wakubali matokeo yaliyotangazwa na tume kuu ya uchaguzi nchini humo. Hata hivyo chama cha upinzani kikiwasii wananchi wasikubaliane na matokeo hayo ya udanganyifu.

Thursday, 18 February 2016

Donald Trumph Criticizes Pope Francis, calls him 'not Chiostian'

Donald Trimph criticizes Pope Francis after he tells him that his not a Christian, during an interview.

“For a religious leader to question a person’s faith is disgraceful. I am proud to be a Christian and as President I will not allow Christianity to be consistently attacked and weakened, unlike what is happening now, with our current President. No leader, especially a religious leader, should have the right to question another man’s religion or faith,”  wrote the Republican presidential candidate on his website.

MORE: Donald Trump Slams Pope Francis, Calls Him ‘Disgraceful’ | Donald Trump, pope francis : Just Jared | http://www.justjared.com/2016/02/18/donald-trump-slams-pope-francis-calls-him-disgraceful/?trackback=tsmclip

Pope Francis questioned Donald Trump's Christianity Thursday over the Republican presidential hopeful's plan to build a wall on the Mexican border, but the Pope himself lives behind massive stone walls.
This happen after he departed from a weeklong tour in which he spoke before millions of people. Pope criticizes Trumph who made hi plan to build a wall and make Mexico to pay for it a centerpiece of his campaign.

"A person who thinks only about building walls, wherever they may be, and not building bridges, is not Christian," Pope Francis said. "This is not in the Gospel."



The Vatican's walls, which do not completely surround the enclave, date back more than 1,000 years, to the time of Pope Leo IV, who commissioned the construction of what is known as the Leonine Wall following the sacking of Old St. Peter's Basilica by Islamic Saracens in 846.

Friday, 12 February 2016

Rais Salva Kiir Amemteua Riek Machar kuwa Makamu wake



Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemteuwa hasimu wake wa kisiasa Riek Machar kuwa makamu wa rais, baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.



“I, Salva Kiir Mayardit, President of the Republic of South Sudan, do hereby issue this Republican Decree for the appointment of Dr. Riek Machar Teny as the first vice President of the Republic of South Sudan,”   Alisema  kiapo hicho siku ya Alhamisi.



 Tangazo la Rais Kiir la jana usiku lilitokana na makubaliano yaliyofikiwa kama sehemu ya muafaka wa amani wa Agosti 2015, ambao ulivunjwa mara kwa mara. Machar, ambaye alikuwa makamu wa rais kuanzia mwaka wa 2005 hadi alipofutwa kazi mwaka wa 2013, na ambaye hajarejea mjini Juba tangu alipokimbilia mafichoni wakati vita vilipozuka Desemba mwaka huo, ameukaribisha uamuzi huo wa Rais Kiir akisema ni hatua ya kusonga mbele katika utekelezaji wa muafaka wa amani. Aliyasema hayo akiwa Ethiopia na haijabainika maramoja ni lini atasafiri kurudi Sudan Kusini ili kuchukua wadhifa huo.
Rik Machar
 Kiir na Machar ni viongozi wa zamani wa waasi walioingia madarakani wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kati ya mwaka wa 1983-2005 baina ya Sudan Kaskazini na Kusini, ambapo Sudan Kusini ilijitenga mwaka wa 2011 na kuwa taifa huru.
Taarifa kutoka Dw Swahili

Tuesday, 2 February 2016

Virusi vya Zika Kujadiliwa WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) leo linafanya mkutano wa dharura kujadili kuenea kwa virusi vya Zika.
Mkutano huo mjini Geneva utajadili iwapo mlipuko wa virusi hivyo unafaa kutangazwa kuwa “dharura ya kimataifa”.

Maafisa wa WHO wamesema mlipuko huo wa Zika unabadilika utoka “hatari ndogo hadi kuwa wa hatari kubwa”.
Katika visa vingi, watu walioambukizwa virusi hivyo vya Zika huwa hawaonyeshi dalili zozote, lakini virusi hivyo vinadaiwa kusababisha maelfu ya watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo Amerika Kusini.

Kutangazwa kwa mlipuko wa sasa wa Zika kuwa “dharura ya kimataifa ya afya ya umma” kutavifanya virusi hivyo kutambuliwa kama hatari kubwa duniani na kupelekea pesa, rasilimali na wataalamu wa kisayansi kutengwa kuangazia tatizo hilo Amerika Kusini na katika maabara kote duniani.
WHO inaangazia sana hasa baada ya kukosolewa kutokana na ilivyoshughulikia mlipuko wa maradhi ya Ebola Afrika Magharibi.
 Kwa Habari Zaidi bbc swahili

Wednesday, 6 January 2016

Bomu la Korea Kaskazini la Tiliwa Shaka.

Bomu la Hydrogen linaloendelea kufanyiwa majaribio huko Korea Kaskazin Lazidi kuongeza mashaka miongoni mwa watu duniani.
ya bomu la nguvu ya maji, maarufu kama bomu la haidrojeni.
BBC SWAHILI  imesema kuwa:
Wataalamu hata hivyo wametilia shaka madai hayo, huku mataifa yenye ushawishi duniani yakisema hatua hiyo ya Korea Kaskazini ni uchokozi.
Tangazo hili limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya ardhi ya kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia. Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikuwa majaribio ya bomu hilo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu.
Mwandishi wa BBC anasema bomu la nguvu ya maji lina uwezo mkubwa wa mlipuko ikilinganishwa na mabomu mengine yenye madini ya Plutonia ambayo Korea kaskazini imefanya majaribio katika miaka ya awali.
Baadhi ya wataalamu wanasema mlipuko uliosikika haukufikia ule unaotokana na bomu la haidrojeni.
Bruce Bennett, mtaalamu katika shirika la Rand Corporation, ni mmoja wa wanaotilia shaka ukweli wa madai ya Pyongyang. Anasema bomu la haidrojeni lingetoa sauti mara 10 kuliko iliyosikika wakati wa mlipuko wa bomu hilo.
Pyongyang imefanya majaribio mengine matatu ya kinyuklia katika eneo kulikofanywa majaribio ya sasa katika kipindi cha miaka kumi. Majaribio ya leo yakithibitishwa, basi itakuwa mara ya nne kwa Korea Kaskazini kufanyia majaribio bomu la haidrojeni tangu 2006.
Taarifa zaidi temdelea


Thursday, 31 December 2015

Buharu: Nigeria Iko Tayari Kufanya Mazungumzo na Boko Haramu.

Rais wa Nigeria Muhamadu Buharu amesema kuwa serukali ya  Nigeria iko tayari kufanya mazungumzo na kundi la kigaidi la Boko Haramu, ili kuwaachia huru  wanafunzi wa kike209 waliotekwa nyara mwezi April 2014.kwenye mji wa Chibok.
Akizungumza jana (30.12.2015) na waandishi wa habari, Rais Buhari amesema wamejiandaa kuzungumza na Boko Haram ili kuwaachia huru wasichana hao waliotekwa mwaka uliopita kwenye mji huo wa kaskazini mashariki, kitendo kilichozuwa lawama kali ulimwenguni na wito wa kuachiwa kwao.
''Bado tumeweka wazi msimamo wetu kwamba kama Boko Haram watatuonyesha uongozi wenye kuaminika na wanatuambia wasichana wale wako wapi, basi tumejiandaa kuzungumza nao bila ya masharti yoyote ya awali,'' alisema Buhari.
Buhari amesema hakuna taarifa madhubuti za kijasusi kuhusu mahali waliko wasichana hao, wala namna afya zao zilivyo na hivyo mazungumzo hayo yanaweza yakaanza tu iwapo maafisa wa Nigeria watathibitisha kuwa wasichana hao wako hai. Ameongeza kusema kuwa wanataka kupata uhakika kwamba wasichana hao wako salama.
Majaribio kama hayo yalishindikana katika utawala uliopita wa Rais Goodluck Jonathan kwa sababu maafisa walikuwa wanazungumza na watu wasio sahihi, lakini Buhari amesema suala la wasichana wa Chibok bado liko kwenye akili za Wanigeria na serikali yao.
Baadhi ya viongozi wa Chibok wiki iliyopita walisema Rais Buhari amewasahau wasichana hao, kwa sababu alitangaza kwamba jeshi la Nigeria limeshinda kiufundi vita dhidi ya Boko Haram. Lakini mashambulizi 48 ya kundi hilo kaskazini mashariki mwa Nigeria, yaliyosababisha vifo vya watu 50, yamefifisha kauli hiyo ya Buhari.
Taarifa zaidi unaweza kufuatilia kupitia DW SWAHILI