Tume ya Uchaguzi ya Nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa urais kwa muula wa tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamis ya Febr. 18, 2016.
Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu. Huku Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye akipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Chama kikuu cha upinzani nchini humo kimeyakataa matokeo hayo wakidai kuwa ni udanganyifu.
Museveni alitangazwa mshindi wakati mpinzani wake mkuu Dkt. Kizza Besigye, akitumikia kifungo cha nyumbani chini ya ulinzi mkali wa polisi. mjini Kampala.
Chama tawala NRM kimewaomba wagombea wote kuheshimu matakwa ya wananchin na kuwaomba wakubali matokeo yaliyotangazwa na tume kuu ya uchaguzi nchini humo. Hata hivyo chama cha upinzani kikiwasii wananchi wasikubaliane na matokeo hayo ya udanganyifu.

Museven Atangazwa Mshindi wa Urais Nchini Uganda
4/
5
Oleh
kwetutz24