Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Saturday, 20 August 2016

Man United Yiadhibu Southampton

Magoli Mawili yaliyofungwa na Ziltan Ibromovich yaliiwezesha timu hiyo kupata ushindi dhidi ya Southampton katika mechi ligi kuu ya Uingereza iliyochezwa hapo jana.
Hivyo Man United kujinyakulia point tatu mkononi dhidi ya southampton.
Kocha Jose Mournho amesifia Paul Pogba moja ya wachezaji waliouzwa kwa gharama kubwa mwaka huu kwa ada ya paundi 89 milioni, alifungua mechi yake ya kwanza baada ya kucheza kwa umahiri mkubwa zaidi ya wachezaji wengine katika timu hiyo, ambapo aliweza kukamilisha pasi (71), alizogusa  (103), huku shots zikiwa  (4).

Wednesday, 20 July 2016

Liverpool Yasajili Kiungo Mpya kutoka Augsburg....

Klabu ya Liverpool imemsajili kiungo mkabaji Ragnar Klavan kwa ada ya paund 4.2 Milion ikiwa kwa mkataba wa miaka mitatu.
Klavern (30) kutoka Estonia ameichezea Augsburg mara 100 na pia amecheza misimu 4 ligi ya Bundesliga, mchezaji huyo akiiambia tovuti ya Klabu ya hiyo alisema kuwa ni heshima kubwa kwake kujiunga na klabu ya Liverpool. na kwamba ilikuwa ni ni ndoto kwake kwa miaka 22 mbele kucheza ligi kuu ya Uingereza.
Liverpool imemsajili mchezaji huyu ili kuziba nafasi za wachezaji waliopatwa na majeraha kama vile Mamadou Sakho na Joe Gomez.

Friday, 1 July 2016

Euro 2016: Portugal Watinga Nusu Fainali

Portugal imefuzu hatua ya Nusu fainali bada ya kuilaza Polanda kwa mikwaju 5 - 3 katika  michuano ya Euro inayofanyika huko nchini Ufaransa, mchezo uliochezwa hapo jana Alhamis.
Ushindi huu imiafanya Portugal kuwa timu ya kwanza kufika hatua ya nusu fainali katika michuani hii ya Euro 2016.
Mchezo huo ulimalizika kwa sara ya goli 1 - 1 ndani ya dakika 120, goli la kwanza katika timu ya Poland likifungwa na Robert Lewandoski katika dk. '2' na hapo baadae kusawazishwa na na Portugal kupitia mchezaji wao Roberto Sanches katika dk. '33'. Na hivyo kwenda hadi hatua ya Penalti ambapo Portugal ilishinda penati 5 - 3 dhidi ya Poland.

Tuesday, 28 June 2016

Liverpool Kuinasa Saini ya Sadio Mane...



Liverool yakamilisha usajili wao baada ya kuinasa saini ya aliyekuwa akiichezea Southampton Sadio Mane kwa ada ya Paundi 34 milioni.
Mane amejiunga na Liverpool kwa mkataba wa Miaka  mitano akiwa ni mchezaji wa tatu kusajiliwa klabuni hapo..
Mane amefunga magoli 21 katika mechi 67 za ligi kuu ya Uingereza baada ya kuiunga na timu yake kwa ada ya paundi milioni 10 akitokea Salzburg mwaka 2014

Wednesday, 22 June 2016

Ibromovic Astaafu Soka La Kimataifa...

Mchezaji wa Sweden Ziltan Ibromovic aliyekuwa akiichezea klabu ya PSG Paris ametangaza rasmi kustaafu sola la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016.
Manchester United imekuwa ikitajwa kuwania saini ya mchezaji huyu baada ya michuano ya Euro 2016.

Tuesday, 21 June 2016

Ghasia South Afrika.....

             Taarifa kutoka BBC DIRA YA DUNIA>>
Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzua ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.
Taarifa ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu, inasema kuwa maafisa wa polisi walifyatuliwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao kwa mawe.
Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC kugombea uchaguzi mwezi Agosti.
Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.
Serikali ya Afrika Kusini imeoamba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo.

Monday, 20 June 2016

FINALI NBA: Cleveland Caveliers watwaa Taji ya NBA - VIDEO

Cleveland Caverliers wametwaa taji kwa mara nyingine tena Baada ya kuifunga Golden State Warriors vika93 - 89 katika finali ya mchezo wa 7 uliochezwa siku ya Jumapili Usiku.
 Huu utakuwa ni ushindi mkubnwa wa kwanza tangu wachukua Championship mwak 1964
Lebron James alitajw kama MVP katika finali hiyo baada ys kushinda vikapu 27



James hakusita kutoa machozi baada ya kuiokoa timu yake na kuipatia timu yake ushindidhdi ya Warriors
"Cleveland, this is for you!" James, an Akron, Ohio, native,walipiga kelele huku wakitokwa na machozi baada ya kupata ushindi huo.
Lebron James alitajwa kama MVP katika finali hiyo baada ya kushinda vikapu 27, rebound 11 na assist 11 kama mchezaji bora katika finali hizo.
Katika FInali hizi hapo mwanzo Golden Warriros waliongoza Finali hizo kwa michezo 3 -1 dhidi ya Cavs.

Uingereza,Wales mwendo mdundo Euro

                           Uingereza na Wales zafuzu hatua ya 16 bora Euro.
                        Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uingereza Jarmie Vardy akijaribu kufunga mbele ya beki Martin Skrtel na  golikipa Matus Kozacik wa Slovakia

Uingereza ,Wales "  mwendo mdundo " , ni kauli pekee inayoweza kutumika kwa timu za Taifa za soka za nchi hizo baada ya ndugu hao wawili kufanikiwa kufuzu kuingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa                              
                            
     Golikipa wa timu ya Tifa ya Uingereza Joe Hart akiokoa hatari langoni mwake.

Uingereza imefuzu michuano hiyo baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana (0 - 0) dhidi ya timu ya taifa ya soka ya Slovakia na kufanikiwa kushika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi B.
Uingereza ambayo iliingia katika mchezo huo wakiwa na nyota wa timu hiyo Jarmie Vardy na Daniel Sturidge katika kikosi cha kwanza hawakufanikiwa kuliona goli la timu pinzani na kushindwa kuongoza kundi hilo.

Kwa Upande wa timu ya taifa ya soka ya Wales, nayo imesonga mbele baada ya kuifunga Urusi kwa magoli 3-0  yaliyofungwa na Aaron Ramsey , N.Taylor na Gareth Bale.
                             
Wachezaji wa timu ya taifa ya Wales wakishangilia goli lao la pili lililofungwa na N.Taylor dhidi ya timu ya taifa  ya Urusi.

Msimamo wa kundi B baada ya mechi za Leo ni kama ifuatavyo :

            Timu                       Pointi.

          1. Wales                       6
          2. Uingereza                5
          3. Slovakia                   4
          4. Urusi.                       1

Kwa matokeo hayo Uingereza itakutana na mshindi wa Pili wa kundi F , na majirani zao Wales watakutana na mshindi wa tatu (Best looser ) wa  kundi A/C au D katika hatua ya 16 bora.
Michezo mingine ya michuano hiyo itaendelea usiku wa leo ambapo Ireland itavaana na Ujerumani , huku Ukraine itakua na kibarua kizito mbele ya Poland, na michezo yote itachezwa kuanzia majira ya saa  Nne kamili  usiku.


Habari na Mzigu Petro.

Sunday, 19 June 2016

Ufaransa , Swiss zafuzu 16 Bora Euro

Wenyeji Ufaransa wang'aa baada ya kufuzu michuano ya Euro 2016,Uswiss wakifuatia.



 Wachezaji wa timu ya taifa ya Switzerland wakishangilia baada ya kutoka suluhu dhidi ya Ufaransa na kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro.


Wenyeji wa michuano ya mataifa ya Ulaya Euro 2016 Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kufuzu katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Ufaransa imefanikiwa kufuzu baada ya kutoka suluhu ya magoli 0-0 dhidi ya Switzerland ambao nao wamefanikiwa kufuzu baada ya kujihakikishia nafasi ya Pili katika kundi A, huku Ufaransa wakiongoza kundi hilo kwa pointi saba.
Katika matokeo mengine ya michezo ya kundi hilo timu ya taifa  ya Albania imeshinda goli 1 - 0 dhidi ya Romania.

Msimamo wa kundi hilo baada ya mechi za mwisho  unasomeka kama ifuatavyo :

      Timu                          Pointi

   1.  Ufaransa                     7
   2.  Switzerland                6
   3.  Albania                       3  
   4.  Romania                     1

   Michezo mingine itapigwa kesho ikihusisha timu za kundi B,ambapo timu ya taifa ya Slovakia itacheza dhidi ya Uingereza huku Urusi wakikutana na Wales ,  michezo yote itapigwa majira ya saa   Nne  kamili usiku.

Habari na Mzigu Petro

 

Friday, 17 June 2016

Finali NBA: Cleveland Yasonga Mbele Kuendelea na Finali ya Mchezo wa 7 - Video

Ikiwa ni finali ya 6 mchezo uliochezwa Alhamis usiku, 16 June. 2106, Lebron James aliongoza kwa vikapu 41, rebound 11 na kuiiwezesha timu yake Cleveland kusonga mbele  kuelekea finali ya mchezo wa saba baada ya kushinda vikapu 115 - 101 dhidi ya Golden State Warriors.

Stephen Curry aliishindia timu yake Warriors vikapu 30 kabla ya kutolewa nje ya mchezo katika mzunguko wa 4 baada ya kufikisha rafu sita alizocheza katika kipindi hicho.
Tazama hapa High lights nzima za Finalo ya 6 ya NBA

Ujerumani, Polandi Ngoma Droo....



Katika michuano ya kuwania kombe la Euro 2016 ikiwa katika kufuzu hatua ya Makundi,  
Ujerumani  na Poland kwa mara ya kwanza wametoka sare ya bila kufungana wakiwa wania kwa nguvu zote kufuzu katika hatua ya makundi katika kundi 'C'.
Kutokana na sare hii nchi hizi mbili sasa wamepanda juu kwa pointi 4 hivyo kumtoa Ukraine katika michuano hiyo akiwa hana pointi.

Wednesday, 15 June 2016

Dunga apigwa Chini....

Mchezaji wa Zamani na Kocha wa Brazili Carlos Dunga ametimuliwa katika timu ya Brazili pamoja na benchi lake la ufundi baada ya kushindwa kuvusha Nchi hiyo kutoka katika hatua ya makundi baada ya kufungwa 1 - 0 na Peru goli lililoelezwa kuwa la mkono na hivyo kutolewa kwenye michuano ya Copa America.

Tuesday, 14 June 2016

Final NBA: Cleveland ya iadhibu Warriros.....

katika finali ya 5 ya mchezo wa NBA kati ya Cleveland Cavallers dhidi ya Golden State Warriors  Lebron James na Kyrie Irving wamekuwa wachezaji wa kwanza wa timu moja kuwa na vikapu 40 kila mmoja katika final moja na Cleveland Cavallerd wakapiga juhudi kuwaadhibu Golden State Warriors 112-97 usiku wa Jumatatu.

Monday, 13 June 2016

Copa America: Brazili Yaondolewa Kwenye Hatua ya Makundi..

Kocha wa Brazili Dunga amesema hanahofu kuhusu kazi yake baada ya timu yake kuondolewa kwenye  michuano ya copa America katika hatua ya Makundi na kusisitiza kuwa  yeye anahofia kufa tu.
Brazili wamepoteza mchezo kwa kufungwa 1 – 0 na Peru hivyo kuondolewa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza  tangu ipite miaka 30.
Lakini washindi hawa mara 5 wa kombe la Dunia wamelalamika kuwa Raul Ruidiaza  aliefunga dk 75 foxboa stadium alishika.
"Alionekana wazi kuwa ameshika"..alisema Dunga
Wachezaji wa  Brazili wammpinga  refa mruguay Adres Cunha lakini aliamua kusimamia maamuzi yake  baada  kushauriana na mwamuzi wanne
Matokeo hayo yanawafanya Brazili walio katika kundi B kuwa nyuma ya  Peru na Ecuador ambao wote wamepita katika hatua ya robo fainali
Peru sasa watacheza na Colombia wakati Ecuador wakikutana na United State ambao ndio wameandaa mshindano hayo.