Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Saturday, 20 August 2016

Man United Yiadhibu Southampton

Magoli Mawili yaliyofungwa na Ziltan Ibromovich yaliiwezesha timu hiyo kupata ushindi dhidi ya Southampton katika mechi ligi kuu ya Uingereza iliyochezwa hapo jana.
Hivyo Man United kujinyakulia point tatu mkononi dhidi ya southampton.
Kocha Jose Mournho amesifia Paul Pogba moja ya wachezaji waliouzwa kwa gharama kubwa mwaka huu kwa ada ya paundi 89 milioni, alifungua mechi yake ya kwanza baada ya kucheza kwa umahiri mkubwa zaidi ya wachezaji wengine katika timu hiyo, ambapo aliweza kukamilisha pasi (71), alizogusa  (103), huku shots zikiwa  (4).

Wednesday, 20 July 2016

Liverpool Yasajili Kiungo Mpya kutoka Augsburg....

Klabu ya Liverpool imemsajili kiungo mkabaji Ragnar Klavan kwa ada ya paund 4.2 Milion ikiwa kwa mkataba wa miaka mitatu.
Klavern (30) kutoka Estonia ameichezea Augsburg mara 100 na pia amecheza misimu 4 ligi ya Bundesliga, mchezaji huyo akiiambia tovuti ya Klabu ya hiyo alisema kuwa ni heshima kubwa kwake kujiunga na klabu ya Liverpool. na kwamba ilikuwa ni ni ndoto kwake kwa miaka 22 mbele kucheza ligi kuu ya Uingereza.
Liverpool imemsajili mchezaji huyu ili kuziba nafasi za wachezaji waliopatwa na majeraha kama vile Mamadou Sakho na Joe Gomez.

Friday, 1 July 2016

Euro 2016: Portugal Watinga Nusu Fainali

Portugal imefuzu hatua ya Nusu fainali bada ya kuilaza Polanda kwa mikwaju 5 - 3 katika  michuano ya Euro inayofanyika huko nchini Ufaransa, mchezo uliochezwa hapo jana Alhamis.
Ushindi huu imiafanya Portugal kuwa timu ya kwanza kufika hatua ya nusu fainali katika michuani hii ya Euro 2016.
Mchezo huo ulimalizika kwa sara ya goli 1 - 1 ndani ya dakika 120, goli la kwanza katika timu ya Poland likifungwa na Robert Lewandoski katika dk. '2' na hapo baadae kusawazishwa na na Portugal kupitia mchezaji wao Roberto Sanches katika dk. '33'. Na hivyo kwenda hadi hatua ya Penalti ambapo Portugal ilishinda penati 5 - 3 dhidi ya Poland.

Tuesday, 28 June 2016

Liverpool Kuinasa Saini ya Sadio Mane...



Liverool yakamilisha usajili wao baada ya kuinasa saini ya aliyekuwa akiichezea Southampton Sadio Mane kwa ada ya Paundi 34 milioni.
Mane amejiunga na Liverpool kwa mkataba wa Miaka  mitano akiwa ni mchezaji wa tatu kusajiliwa klabuni hapo..
Mane amefunga magoli 21 katika mechi 67 za ligi kuu ya Uingereza baada ya kuiunga na timu yake kwa ada ya paundi milioni 10 akitokea Salzburg mwaka 2014

Wednesday, 22 June 2016

Ibromovic Astaafu Soka La Kimataifa...

Mchezaji wa Sweden Ziltan Ibromovic aliyekuwa akiichezea klabu ya PSG Paris ametangaza rasmi kustaafu sola la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016.
Manchester United imekuwa ikitajwa kuwania saini ya mchezaji huyu baada ya michuano ya Euro 2016.

Tuesday, 21 June 2016

Ghasia South Afrika.....

             Taarifa kutoka BBC DIRA YA DUNIA>>
Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzua ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.
Taarifa ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu, inasema kuwa maafisa wa polisi walifyatuliwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao kwa mawe.
Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC kugombea uchaguzi mwezi Agosti.
Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.
Serikali ya Afrika Kusini imeoamba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo.