Monday, 20 June 2016

Uingereza,Wales mwendo mdundo Euro

                           Uingereza na Wales zafuzu hatua ya 16 bora Euro.
                        Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uingereza Jarmie Vardy akijaribu kufunga mbele ya beki Martin Skrtel na  golikipa Matus Kozacik wa Slovakia

Uingereza ,Wales "  mwendo mdundo " , ni kauli pekee inayoweza kutumika kwa timu za Taifa za soka za nchi hizo baada ya ndugu hao wawili kufanikiwa kufuzu kuingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa                              
                            
     Golikipa wa timu ya Tifa ya Uingereza Joe Hart akiokoa hatari langoni mwake.

Uingereza imefuzu michuano hiyo baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana (0 - 0) dhidi ya timu ya taifa ya soka ya Slovakia na kufanikiwa kushika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi B.
Uingereza ambayo iliingia katika mchezo huo wakiwa na nyota wa timu hiyo Jarmie Vardy na Daniel Sturidge katika kikosi cha kwanza hawakufanikiwa kuliona goli la timu pinzani na kushindwa kuongoza kundi hilo.

Kwa Upande wa timu ya taifa ya soka ya Wales, nayo imesonga mbele baada ya kuifunga Urusi kwa magoli 3-0  yaliyofungwa na Aaron Ramsey , N.Taylor na Gareth Bale.
                             
Wachezaji wa timu ya taifa ya Wales wakishangilia goli lao la pili lililofungwa na N.Taylor dhidi ya timu ya taifa  ya Urusi.

Msimamo wa kundi B baada ya mechi za Leo ni kama ifuatavyo :

            Timu                       Pointi.

          1. Wales                       6
          2. Uingereza                5
          3. Slovakia                   4
          4. Urusi.                       1

Kwa matokeo hayo Uingereza itakutana na mshindi wa Pili wa kundi F , na majirani zao Wales watakutana na mshindi wa tatu (Best looser ) wa  kundi A/C au D katika hatua ya 16 bora.
Michezo mingine ya michuano hiyo itaendelea usiku wa leo ambapo Ireland itavaana na Ujerumani , huku Ukraine itakua na kibarua kizito mbele ya Poland, na michezo yote itachezwa kuanzia majira ya saa  Nne kamili  usiku.


Habari na Mzigu Petro.

Related Posts

Uingereza,Wales mwendo mdundo Euro
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR