Sunday 19 June 2016

Ufaransa , Swiss zafuzu 16 Bora Euro

Wenyeji Ufaransa wang'aa baada ya kufuzu michuano ya Euro 2016,Uswiss wakifuatia.



 Wachezaji wa timu ya taifa ya Switzerland wakishangilia baada ya kutoka suluhu dhidi ya Ufaransa na kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro.


Wenyeji wa michuano ya mataifa ya Ulaya Euro 2016 Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kufuzu katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Ufaransa imefanikiwa kufuzu baada ya kutoka suluhu ya magoli 0-0 dhidi ya Switzerland ambao nao wamefanikiwa kufuzu baada ya kujihakikishia nafasi ya Pili katika kundi A, huku Ufaransa wakiongoza kundi hilo kwa pointi saba.
Katika matokeo mengine ya michezo ya kundi hilo timu ya taifa  ya Albania imeshinda goli 1 - 0 dhidi ya Romania.

Msimamo wa kundi hilo baada ya mechi za mwisho  unasomeka kama ifuatavyo :

      Timu                          Pointi

   1.  Ufaransa                     7
   2.  Switzerland                6
   3.  Albania                       3  
   4.  Romania                     1

   Michezo mingine itapigwa kesho ikihusisha timu za kundi B,ambapo timu ya taifa ya Slovakia itacheza dhidi ya Uingereza huku Urusi wakikutana na Wales ,  michezo yote itapigwa majira ya saa   Nne  kamili usiku.

Habari na Mzigu Petro

 

Related Posts

Ufaransa , Swiss zafuzu 16 Bora Euro
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR