Monday 13 June 2016

Copa America: Brazili Yaondolewa Kwenye Hatua ya Makundi..

Kocha wa Brazili Dunga amesema hanahofu kuhusu kazi yake baada ya timu yake kuondolewa kwenye  michuano ya copa America katika hatua ya Makundi na kusisitiza kuwa  yeye anahofia kufa tu.
Brazili wamepoteza mchezo kwa kufungwa 1 – 0 na Peru hivyo kuondolewa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza  tangu ipite miaka 30.
Lakini washindi hawa mara 5 wa kombe la Dunia wamelalamika kuwa Raul Ruidiaza  aliefunga dk 75 foxboa stadium alishika.
"Alionekana wazi kuwa ameshika"..alisema Dunga
Wachezaji wa  Brazili wammpinga  refa mruguay Adres Cunha lakini aliamua kusimamia maamuzi yake  baada  kushauriana na mwamuzi wanne
Matokeo hayo yanawafanya Brazili walio katika kundi B kuwa nyuma ya  Peru na Ecuador ambao wote wamepita katika hatua ya robo fainali
Peru sasa watacheza na Colombia wakati Ecuador wakikutana na United State ambao ndio wameandaa mshindano hayo.

Related Posts

Copa America: Brazili Yaondolewa Kwenye Hatua ya Makundi..
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR