Wednesday 15 June 2016

Dunga apigwa Chini....

Mchezaji wa Zamani na Kocha wa Brazili Carlos Dunga ametimuliwa katika timu ya Brazili pamoja na benchi lake la ufundi baada ya kushindwa kuvusha Nchi hiyo kutoka katika hatua ya makundi baada ya kufungwa 1 - 0 na Peru goli lililoelezwa kuwa la mkono na hivyo kutolewa kwenye michuano ya Copa America.

Shirikisho la Soka nchini humo CBF limemfukuza kocha huyo pamoja na benchi lake la ufundi na kusema kuwa litateuwa watu wengine kuongoza timu hiyo.
Kocha huyo ambae alisema kuwa haogopi kutimuliwa baada ya kufungwa na Peru, tangu Dunga awe kocha wa Brazili timu hiyo mara mbili, timu hiyo imekuwa ikishindwa kufanya vizuri katika michuano ya kopa America 2015 ilipotolewa katika hatua ya nusu fainali na sasa 2016 kwa kutolewa kwenye atua ya makundi.

Related Posts

Dunga apigwa Chini....
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR