Friday, 12 February 2016

Rais Salva Kiir Amemteua Riek Machar kuwa Makamu wake



Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemteuwa hasimu wake wa kisiasa Riek Machar kuwa makamu wa rais, baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.



“I, Salva Kiir Mayardit, President of the Republic of South Sudan, do hereby issue this Republican Decree for the appointment of Dr. Riek Machar Teny as the first vice President of the Republic of South Sudan,”   Alisema  kiapo hicho siku ya Alhamisi.



 Tangazo la Rais Kiir la jana usiku lilitokana na makubaliano yaliyofikiwa kama sehemu ya muafaka wa amani wa Agosti 2015, ambao ulivunjwa mara kwa mara. Machar, ambaye alikuwa makamu wa rais kuanzia mwaka wa 2005 hadi alipofutwa kazi mwaka wa 2013, na ambaye hajarejea mjini Juba tangu alipokimbilia mafichoni wakati vita vilipozuka Desemba mwaka huo, ameukaribisha uamuzi huo wa Rais Kiir akisema ni hatua ya kusonga mbele katika utekelezaji wa muafaka wa amani. Aliyasema hayo akiwa Ethiopia na haijabainika maramoja ni lini atasafiri kurudi Sudan Kusini ili kuchukua wadhifa huo.
Rik Machar
 Kiir na Machar ni viongozi wa zamani wa waasi walioingia madarakani wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kati ya mwaka wa 1983-2005 baina ya Sudan Kaskazini na Kusini, ambapo Sudan Kusini ilijitenga mwaka wa 2011 na kuwa taifa huru.
Taarifa kutoka Dw Swahili

Related Posts

Rais Salva Kiir Amemteua Riek Machar kuwa Makamu wake
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR