Rais wa Nigeria Muhamadu Buharu amesema kuwa serukali ya Nigeria iko tayari kufanya mazungumzo na kundi la kigaidi la Boko Haramu, ili kuwaachia huru wanafunzi wa kike209 waliotekwa nyara mwezi April 2014.kwenye mji wa Chibok.
Akizungumza jana (30.12.2015) na waandishi wa habari, Rais Buhari amesema wamejiandaa kuzungumza na Boko Haram ili kuwaachia huru wasichana hao waliotekwa mwaka uliopita kwenye mji huo wa kaskazini mashariki, kitendo kilichozuwa lawama kali ulimwenguni na wito wa kuachiwa kwao.
''Bado tumeweka wazi msimamo wetu kwamba kama Boko Haram watatuonyesha uongozi wenye kuaminika na wanatuambia wasichana wale wako wapi, basi tumejiandaa kuzungumza nao bila ya masharti yoyote ya awali,'' alisema Buhari.
Buhari amesema hakuna taarifa madhubuti za kijasusi kuhusu mahali waliko wasichana hao, wala namna afya zao zilivyo na hivyo mazungumzo hayo yanaweza yakaanza tu iwapo maafisa wa Nigeria watathibitisha kuwa wasichana hao wako hai. Ameongeza kusema kuwa wanataka kupata uhakika kwamba wasichana hao wako salama.
Majaribio kama hayo yalishindikana katika utawala uliopita wa Rais Goodluck Jonathan kwa sababu maafisa walikuwa wanazungumza na watu wasio sahihi, lakini Buhari amesema suala la wasichana wa Chibok bado liko kwenye akili za Wanigeria na serikali yao.
Baadhi ya viongozi wa Chibok wiki iliyopita walisema Rais Buhari amewasahau wasichana hao, kwa sababu alitangaza kwamba jeshi la Nigeria limeshinda kiufundi vita dhidi ya Boko Haram. Lakini mashambulizi 48 ya kundi hilo kaskazini mashariki mwa Nigeria, yaliyosababisha vifo vya watu 50, yamefifisha kauli hiyo ya Buhari.
Taarifa zaidi unaweza kufuatilia kupitia DW SWAHILI
Buharu: Nigeria Iko Tayari Kufanya Mazungumzo na Boko Haramu.
4/
5
Oleh
kwetutz24