Thursday 31 December 2015

Kamanda Suleiman Kova Astaafu Rasmi

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam Suleiman Kova amestaafu rasmi hivi leo Dec. 31, 2015 baada yakulitumikia ueshi hilo kwa mda mrefu sasa.

Akizungumza na watanzania hivi leo asubuhi kupitia kipindi cha Kumakucha cha ITV, amesema kuwa mkataba wake na jeshi la polisi nchin umekwisha hivyo analaimika kukaa pembeni na kumwachia majukumu hayo mtu mwingine.
Mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi”, alisema Kamanda Kova.
Kamanda Kova alikuwa Kamanda w Kanda Maalum Dar es Salaam na kwa mujibu wake ameweza kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa tangu aianza kazi yake.

Related Posts

Kamanda Suleiman Kova Astaafu Rasmi
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR