Kambi ya Dadaab imekuwa kimbilio la wasomalia zaidi
ya 300, 000.\
Rais Hassam Sheik Mohamed ameiambia BBC
kuondolewa kwa lazima kwa wakimbizi hao haikuwa maslahi ya taifa lolote..
Kenya imesema inataka kufunga kambi kutokana na
hali usalama, wakisema kuwa mashambulizi katika ardhi yao yamekuwa yakilengwa
kwenye kambi hiyo..
Kenya haikutilia maanani vitisho vile vilivyo
fanyika mwezi Aprili kufuatia mashambulizi ya vifo vya wanamgambo wa kundi la
kisomali la Al- shabaab Kilomita 100 kutoka eneo la chuo..
Kundi la al-Qaeda linalohusishwa na mashambulzi
hayo limekuwa likifanya mashambulio kadhaa nchini Kenya katika miaka ya hivi
karibuni.
Akizungumza na BBC Rais Maohameid amesema kwamba,
Uongozi unatakiwa kufanya makubaliano
katika kutafuta njia bora ya kuwarudisha watu hao katika taifa lao na
katika hali inayoeleweka kulingana na sheria za kimataifa. Hatutaki mahusiano
yetu yaathiriwe na Kenya,
Aliendelea kusema kuwa Kenya ilikuwa na msaada
mkubwa katika kuwahifandhi wakimbizi kwa kipindi cha mda mrefu sasa na imekuwa
ikijituma katika kuwarejesha watu wa taifa lake.
Daadab ilianzishwa mwaka 1991 kwa wanafamilia
waliokuwa wakiikimbia Somalia kutoka na migogoro na baadhi ya watu wamekuwa
wakiishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20.
Rais Wa Somalia Ataka Njia Muafaka kuwarudisha wakimbizi katika Taifa lake...
4/
5
Oleh
kwetutz24