Saturday 23 January 2016

Liverpool Yapata Ushindi dhidi ya Norwich City

Norwich City wakiwa wenyeji wa mchezo huo imepokea kipigo cha magoli 5 - 4 kutoka kwa Liverpool, katika mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza.
Roberto Firmino aliifungia Liverpool katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo na kuifanya timu yake itangulie mbele kwa goli moja dhidi ya Norwich. Mbokani Bezua(Norwich) alisaazisha goli hilo katika dk.29 huku Steven Naismith akiongeza goli la pili katika dk. 41. na hivyo kuiweka timu yao Norwich kuwa mbele kwa magoli mawili kwa moja.
Wes Hoolahan(Norwich) akiongeza goli la tatu katika dk. 54 upitia penati, kabla ya Jordan Henderson na Firmino kufunga katika dk. 55 na 63..
 James Milner(Liverpool) aliongezea goli la nne katika dk. 75 lakini Sebastian Bassong(Nnorwich) alisawazisha katika dk,. 90 ya kipindi cha pili, na katika dakika hiyohiyo Liverpool ilifanikiwa kuongeza goli la tano, goli likifungwa kupitia Laliana. Na hivyo kuipatia ushindi Liverpool magoli 5 - 4 dhidi ya Norwich City.

Related Posts

Liverpool Yapata Ushindi dhidi ya Norwich City
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR