Tuesday 15 March 2016

Vigogo watatu Rahco Wafikishwa Kortini

Mkurugenzi Mkuu wa zamanni wa Kampuni ya Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania RAHCO Benardhard Tito pamoja na wenzake wawili, wamefikishwa kortini katika Mahakama Kuu ya Kisutu Mkazi jijini Dar es Salaam,  wakikabiliwa na mashtaka manne.

Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka haya, Matumizi mabaya ya madaraka, Kuhujumu uchumi, Kula njama na kusababishia serikali hasara ya dola za Marekani 527, 540.
Washatakiwa wawili ni mfanyabiashara na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild Property Limited(SouthAfrika)  anayedaiwa kuwa dalali wa zabuni, Kanji Mwinyijuma na aliyekuwa Katibu na mwanansheria  wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe.
Washitakiwa hao watatu walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba huku pembeni akiwemo wakili Mkuu wa serikali, Timon Vitalis, Maghela Ndimbo na Janeth Machulya kutoka Takukuru.
Mashtaka hayo yakiongozwa na Wakili Vitalis Timon, washtakiwa wote watatu kwa nyakati tofauti kati ya September mosi 2014 na September 30, 2015 mkoa wa Dar es Salaam, washtakiwa hawa watatu walikula njama   ya kutenda makosa hayo chini ya Sheria ya Kuzia na Kupambana na Rushwa.
Katika Kesi hiyo, Februari 27, 2015 Tito mwaka jana katika ofisi za kampuini hiyo zilizopo Ilala Dar es Salaam, alitumia vibaya madaraka baada ya kuidhinisha kampuni ya Rothschild (South Africa) Property kuwa mshauri katika mpango wa ujenzi wa Reli ya Kati, bila kuidhinishwa na Bodi ya Zabuni ya Kampuni hiyo.
Machi 12, 2014 katika ofisi za Rahco, Tito na Massawe wanadaiwa kuwa walisaini barua ya kuikubali kampuni ya Rothschild (South Africa) Property kutoa huduma ya ushauri wa kifedha katika ujenzi wa Reli ya Kati bila kuidhinishwa na bodi.
Aidha, Kati ya Machi 12 na Mei 20, 2015 wanadaiwa kuwa, wakiwa ofisini kwao, waliacha majukumu yao kwa kushindwa kuwasilisha mkataba wa Kampuni ya Rothschild kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
kati ya Mei 20 na Juni 20, 2015, walishindwa kuwasilisha nakala za mkataba wa makubaliano wa kampuni hiyo na kampuni ya Rahco, kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkaguzi wa ndani na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Pia washitakiwa hao kwa nyakati tofauti, kati ya Machi Mosi na Septemba 30, mwaka jana washitakiw wote watatu kwa pamoja walikubaliana kuidhinisha makubaliano ya kampuni hiyo katika masuala ya kiushauri na kusababishia kampuni hasara ya dola za Kimarekani 527, 540, ambazo zilishalipwa kiwango cha awali benki.
Agosti 18, 2015, Tito alitelekeza majukumu yake na alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa zabuni ya upendeleo kwa kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China Construction Corporation. Inadaiwa katika zabuni hiyo, kampuni ilipewe kazi ya ujenzi wa reli ya kilometa mbili yenye kiwango cha kisasa kuanzia Soga ikiwa na thamani ya dola za Marekani 2, 312, 229.39 bila kuidhinishwa na Bodi ya Zabuni ya Rahco.
Washitakiwa wote watatu hawakuruhusiwa kujibu mashtaka hayo kwakuwa Mhakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu. Uamuzi wa dhamana utatolewa siku ya Ijumaa.

Related Posts

Vigogo watatu Rahco Wafikishwa Kortini
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR