Tuesday 22 December 2015

Dr.MAGUFULI AMSIMAMISHA AFISA RAHCO

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania RAHCO, Mhandisi Benhadard Tito.  baada- ya kutuhumiwa   kukiuka taratibu za manunuzi katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati..
Magufuli alichukua hatua hiyo kali baada ya mkutano na wadau wanaohusika na ujenzi wa reli ya kisasa yaani “Standard Gauge”
Uchunguzi wa kimsingi unaelekezwa kwa utoaji wa zabuni hiyo inayokisiwa kugharimu takriban dola milioni $14.

Sasa Magufuli al maarufu "The Bulldozer" ameiagiza mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.
Si hao tu walioathirika na amri hiyo ya rais Magufuli, bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) pia imevunjiliwa mbali.

Related Posts

Dr.MAGUFULI AMSIMAMISHA AFISA RAHCO
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR