Tuesday, 22 December 2015

jeshi La Polisi Linawashikilia Askari 6 kwa Mauaji

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia Askari sita baada ya kuua watuhumiwa wawili wa Ujangili huku mtuhumiwa mmoja akiendelea kusakwa.
Kamanda wa Kikosi Sulemani Kova amesema wawili kati ya hao sita walikuwa ni Polisi huku wane wakiwa ni Askari wa wanyama pori Kikosi Kazi Maalum cha kuzuia ujangili..
wawali hao  waliofariki walitambulika kwa majina  Moja akiwa Yasini Rashidi (46) aliyekuwa Mkazi wa Mabibo pamoja na Samson Masigara(46) aliyekuwa mkazi wa Mbezi.
"Taarifa za mwanzo  zinasema kuwa Askari hawa pamoja na mwenzao walikuwa wakiwafuatilia watu wawili kwa tuhuma za kujihusisha na  ujangili....na msako ulipangwa kufanyika Dec. 19
Uchunguzi ukabaini kuwa kulikuwa na utata tangu tuko hili linafabyika wakati wakiwasaka wawili hawa mpaka kifo ndio maana tumeamua kuwashikilia ilikupata  ukweli wa vifo hivi na uhalali wa nguvu iliyotumika.. alisema
Hata hhivto askari hao walishindwa kutoa taarifa za kutosha na ukweli kuhusu tukio hilo kwakuwa siku hiyo ya tukio kulikuwa hakuna majibizano ya risasi baina yao na watuhmiwa hao wawili wa ujangili..

Related Posts

jeshi La Polisi Linawashikilia Askari 6 kwa Mauaji
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR