Aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF hivi punde ametengaza rasmi kujiuzulu rasmi katika nafasi ya uenyekiti katika chama hicho, hii inafuatia baada ya mwenyekiti akiongea na vyombo vya habari siku ya leo,
amesema kuwa, amekerwa
na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama
shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja
huo.
pia akiongeza kuwa UKAWA ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa
kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba
nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa
wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania
uongozi wa nchi kupitia umoja huo.
Na baada hapo Prof. Lipumba amesema kwamba pamoja na kujiuzulu yeyey atabaki kuwa mwananchama wa kawaida katika chama hicho na sio mwenyekiti tena. na pia atajihusisha na maswala ya kitaaluma na ushauri wa maswala ya uchumi na maendeleo.
tazama vidoe hii hapa chini kutoka Jamii forum
akitoa sababu za kujiuzulu kwake
Prof. Lipumba
Breaking News; Prof. Lipumba ametangaza leo rasmi kujiuzulu Uenyikiti wa Chama cha Wananchi CUF
4/
5
Oleh
kwetutz24