Tuesday 19 January 2016

Gazeti la Mawio lafutwa kwenye orordha ya magazeti Nchini.

Waziri wa Habari, michezo, sanaa na utamaduni Nape Nnauye amelifungia rasmi gazeti maarufu hapa nchini Mawio ikiwa pamoja na kufungia shughuli zote za usambazaji na uchapishaji wa gazeti hilo. Moaja ya sabau alizo toa waziri huyo juu ya kulifuta gazeti hilo kwenye orodha ya magazeti hapa nchini ni kuwa wahariri wa gazeti hilo wamekuwa na kiburi mbele ya serikali pale wanapoambiwa wajitetee kuhusu habari wanazo ziandika.
Akizungumza na waandhishi wa habari siku hiyo, Nape alisema kuwa sharia ya magazeti ya mwaka 1976 sura ya 229 kifungu cha 25 kinampa mamlaka ya kulifungia gazeti hilo, na kwanzia  terehe 15 January mwaka huu amelifuta gazeti hilo kwenye orodha ya msajili ikiwa pamoja na kulipiga marufuku kuchapisha kwenye mitandao .
 Waziri aliendelea kwa kutaja sababu ya serikali kufikia hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo, ni baada ya ofisi ya msajili wa magazeti kuwaandikia barua wahariri wa gazeti hilo,kwa kuwataka wasahihishe makosa yao tangu 2013 jambo analodai kuwa wahariri wake wamekuwa wakiijibu majibu mabaya serikali.
"Yaani wahariri wa hili gazeti tangu mwaka 2013 tunawaambia wabadilishe aina ya uandishi wa habari lakini wakawa wanaijibu serikali majibu mabaya na wakawa wanaendelea kuandika habari ya uchochezi na kuharibu amani ya nchi,”
Pamoja na hayo Waziri amevitaka vyombo vya habari pamoja na wahariri kuzingstia sharia na kanunu za taratibu za nchi kwa kuandika habari zenye kufuata weledi.
Baada ya tukio hilo. Wahariri wa Gazeti la Mawio Saimon Mkina na Jabir Idrissa  walisakwa na jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam, ambapo walivamia ofisi mbili za gazeti hilo kwa kosa la kuandika kwenye gazeti hilo toleo 152 ya Alhamisi ya tarehe 13 January mwaka huu,japo kuwa waliwakosa.

Kichwa cha Habari cha Gazeti hilo kilisema, "Machafuko Yaja Zanzibar.

Aidha mmoja wa wamiliki wa gazeti hilo ambae hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa amezipokea taarifa za kufungiwa kwa gazeti hilo, ila wako mbioni kulifufua gazeti lilokufa, iliwaewndelee na kazi zilizokuwa zikifanywa na gazeti lilofungwa.











Related Posts

Gazeti la Mawio lafutwa kwenye orordha ya magazeti Nchini.
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR