Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Monday, 21 March 2016

Dk. Shein Awa Rais wa Zanzibar.

Katika uchaguzi wa marudio ulifanyika visiwani Zanzibar hapo jana March 20, 2016, Mgombea wa kiti cha uraisi kupitia CCM Dk. Ali Mohammed Shein ameshinda nafasi ya Urais kwa kura 299, 982 sawa na asilimia 91.4 ya kura halali 328, 327 .
Matokeo hayo ya uchaguzi yametangazwa hivi leo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha
Uchaguzi huo umefanyika baada ya Kufutwa kwa uchaguzi wa mwanzo ulofanyika Oct.25, 2015 kwa kile kilichodhaniwa na Kiongozi wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, Jecha kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi huo.
Tazama video hapa chini Jecha akitangaza matokeo ya uchaguzi Zanzibar.

Friday, 22 January 2016

Jecha Atangaza Tarehe ya Uchaguzi wa Marudio Zanziber

Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) ametangaza tarehe 20 March kuwa ndio siku ya Uchaguzi wa marudio Zanzibar. 
Jecha alise,ma kuwa uchaguzi huo utahusisha Rais wa Zanzibar, wajumbe wa baraza la wawakilishi pamoja na adiwani.
Hapo mwanzo jecha litangaza kufutwa kwa matokeo ya uchacuzi Zanzibar kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi huo wa October 25. Hata hivyo mwenyekiti huyo hakutaja ni kifungu gani cha sharia kilicho mruhusu kutangaza uchaguzi uo wa marudio.
Ni siku takribani 90 zimepita tangu kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar October 28, mwaka jana, taratibu za kufuta uchaguzi huo zilihusisha wagombea wote wawili wa urais, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na katibu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
Tayari Maalim Seif ameshajitoa kwenye mazungumzo hayo yaliyohusisha vikao tisa. Nae Naibu katibu wa CUF Bara, Magdallena Sakaya hakuwa tayari kuzuzngumzia suala hilo kwakuwa alichelewa kupata Taarifa hizo.

Friday, 15 January 2016

Lowassa: Najiandaa kwa Uchaguzi 2020

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amesema kuwea yuko tayari kwa mara nyingine tena kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Maneno haya aliyasema wakati akizungumza na jopo la wafanya biashara wakuu Kariakoo jijini Dar es Salaam walio kwenda kumtembelea ofisini kwake.
Lowassa ambae alileta upinzani mkubwa kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana baada ya kuhamia CHADEMA  alipata kura za wananchi 6 mil. alisema  kuwa maadnalizi ya uchaguzi ya uchagui meingine yameshaanza na akawataka wafuasi wake kutokata tama.
"Niko salama, niko fit na nina morali" alisema Lowassa baada ya wapinzani wake kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM. kudai kuwa anamatatizo ya kiafya.
Aliendelea kusema kuwa hato kata tama na ataendelea kugombea kwa kuwa watu wananmpenda.
akisema kuwa katiba ilikua mbaya ndio maana aliamua kukaa kimya ilikuleta usalama ndani ya nchi angeamua kupinga matokeo hayo basi watu wange chinjana na wengine kupoteza maisha na hata maafa yangetokea.
Taarifa zaidi>>>>MWANANCHI

Wednesday, 16 December 2015

Kubenea Apandishwa Kortini

Mbunge wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea amepandishwa kizimnani katika mahakama ya Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam hapo jana  Kwa tuhuyma za kutumia lugha chafu dhidi ya mbunge wa Kinondonii Paul Makonda.
Kubenea akitetewa na Mawakili sita alikataa tuhuma hizo dhidi yake ya kwamba alimwita Makonda kuwa "wewe ni mpumbavu, mjinga, " . Kubenea alipewa dhamana na kuachiwa huru na kesi hiyo imeahirishwa mpakia Dec. 29.

Thursday, 10 December 2015

Magafuli Atangaza Baraza la Mawaziri

Rais w Jamhuri ya Muunano wa Tanzana Dr. Magfuli Ameteua rasmi  Baraza jipya la Mawaziri Hivi Leo jijini Dar es Salaam.
Tizaama Video hii wakati Magufuli akiteua araza La Mwwaziri.

Itazame Orodha nzima ya Mawari.
 

Baraza la Mawaziri





 

Tuesday, 3 November 2015

Tb Joshua Ametua Jijini Dar es salama Kushudua Kuapishwa kwa Rais Mteule hapo Alhamis Tareh. 05 Nov.

Mhubiri na nabii TB Joshua wa Kanisa la Church of All Nation ametua jijini Dar Es Salaam hivi leo Kwa ajili Ya Kushuhudia kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo Alhamis Tareh. 05.

Alipo tua kutoka kwenye uwanja wa ngege wa Mwalimu Julious Nyerere alikwenda moja kwa moja mpaka ikulu kumsalimiaRais Kikwete na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi kwa uhuru na amanni, pia Tb Joshua amempongeza Kikwete kwa uongozi wake ns kwa kumpata mrithi wake Dr.John Pombe Magufuli.

Tb Joshua atakuwepo Jijini Dar es Salaama akishuhudia kuapishwa kwa Rais mteule hapo tareh. 05.Nov. mwaka huu.