Monday 21 March 2016

Dk. Shein Awa Rais wa Zanzibar.

Katika uchaguzi wa marudio ulifanyika visiwani Zanzibar hapo jana March 20, 2016, Mgombea wa kiti cha uraisi kupitia CCM Dk. Ali Mohammed Shein ameshinda nafasi ya Urais kwa kura 299, 982 sawa na asilimia 91.4 ya kura halali 328, 327 .
Matokeo hayo ya uchaguzi yametangazwa hivi leo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha
Uchaguzi huo umefanyika baada ya Kufutwa kwa uchaguzi wa mwanzo ulofanyika Oct.25, 2015 kwa kile kilichodhaniwa na Kiongozi wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, Jecha kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi huo.
Tazama video hapa chini Jecha akitangaza matokeo ya uchaguzi Zanzibar.

Related Posts

Dk. Shein Awa Rais wa Zanzibar.
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR