Friday 22 January 2016

Jecha Atangaza Tarehe ya Uchaguzi wa Marudio Zanziber

Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) ametangaza tarehe 20 March kuwa ndio siku ya Uchaguzi wa marudio Zanzibar. 
Jecha alise,ma kuwa uchaguzi huo utahusisha Rais wa Zanzibar, wajumbe wa baraza la wawakilishi pamoja na adiwani.
Hapo mwanzo jecha litangaza kufutwa kwa matokeo ya uchacuzi Zanzibar kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi huo wa October 25. Hata hivyo mwenyekiti huyo hakutaja ni kifungu gani cha sharia kilicho mruhusu kutangaza uchaguzi uo wa marudio.
Ni siku takribani 90 zimepita tangu kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar October 28, mwaka jana, taratibu za kufuta uchaguzi huo zilihusisha wagombea wote wawili wa urais, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na katibu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
Tayari Maalim Seif ameshajitoa kwenye mazungumzo hayo yaliyohusisha vikao tisa. Nae Naibu katibu wa CUF Bara, Magdallena Sakaya hakuwa tayari kuzuzngumzia suala hilo kwakuwa alichelewa kupata Taarifa hizo.

Related Posts

Jecha Atangaza Tarehe ya Uchaguzi wa Marudio Zanziber
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR