Thursday 15 October 2015

Christino Ronaldo na Kiatu cha Dhahabu, Vip Kuhusu Kustaafu kwa Soka Lake......

Christiano Ronaldo amejinyakulia tena kiatu cha dhahabu kwa mara ya nne baada ya kufunga idadi ya magoli 48 katika michezo 35 ya Ligi Kuu ya Hispania, La Liga. Wakati akipokea kiatu hicho akiwa Madrid, Ronaldo alichukizwa na uvumi juu yake kuhusu yeye kurudi katika timu ya Manchester United na kusema na akasema kuwa "Hakuna ajuaye nini kitatokea mwaka ujao".
Kapteni huyu wa Ureno ameanza kuichezea Real Madrid mwaka2009 akitokea  Manchester Untied wa ada ya paund 80 milli.
Juu ya mpango mzia wa kustaafu kwa mchezaji huyu amesema kuwa ataendelea kuichezea timu hiyo mpaka atakapo fikisha miaka 40. na angependa kuendeleza kazi yake akiwa katika timu hiyo, na kusema "Real Madrid ni timu bora Duniani"
"Ninataka ushindi zaidi. bado najihisi kijana na niko vizuri, nina miaka30  ningependa kuendelea kucheza kwa miaka 5 au miaka 6 zaidi na kwa wakati huo ningependa kuweka mambo sawa na kudumish kiwango cha msimu wa hivi karibuni. Nafahamu inakuwa ni vigumu wakati wote, lakini kichwani mwangu nadhani inawezekana".

Related Posts

Christino Ronaldo na Kiatu cha Dhahabu, Vip Kuhusu Kustaafu kwa Soka Lake......
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR