Wednesday 13 April 2016

Real Madrid, Man City Zatinga Nusu Finali..


Real Madrid imetinga nusu finali hapo jana baada ya kuilaza Wolfsburg magoli 3 kwa 0 katika nusu finali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Christiano Ronaldo aliifungia timu yake hat trick, mabao hayo yalifungwa katika dakika ya '16', '17', na '77' ya mchezo huo, dhidi ya wapinzani wao na hivyo kuifanya timu yake isonge mbele katika hatua ya nusu finali.
kwingineko  barani Ulaya, nao Manchester City wamesonga mbele katika hatua ya nusu finali baada ya kuitandika PSG ya Paris, Ufaransa goli 1 kwa 0 katika michuano ya klabu bingwa Ulaya. Bao hilo likifungwa kupitia mchezaji wao Kelvin De Bruyne katika dakika ya '76'.

Related Posts

Real Madrid, Man City Zatinga Nusu Finali..
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR