Monday 19 October 2015

Ommy Dimpozi Kudondosha Album yake Mwishoni Mwa Mwaka Huu

Msanii wa bongo flava Ommy Dimpoz ametangaza rasmi kuachia album yake mpya mwezi December mwaka huu. Mwishoni mwa mwaka jana msanii huyu aliahidi kudondosha album hiyo mapema kabisa  kipindi cha valentine day lakini kutokana na harakati za uchaguzi na kampeni za kisisasa akashindwa kuachia album hiyo.
Ommy Dimpozi alisema;
“So far nina nyimbo nyingi ambazo nimezirekodi, kwasababu kama nilivyoahidi tangia mwanzo nilikuwa na mpango wa kutoa album kwaajili ya mashabiki, ambayo sasa hivi kutokana na vuguvugu la uchaguzi ningekuwa tayari nimeshatoa lakini kutokana na kuupisha uchaguzi nimefikiria kuiahirisha hadi December.”
Ommy Dimpozi hivi karibuni ameweza kujinyakulia tuzo yake ya Afrimma kama Best New Comer2015.

Related Posts

Ommy Dimpozi Kudondosha Album yake Mwishoni Mwa Mwaka Huu
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR