Monday 19 October 2015

Maelfu ya Wahamiaji Wakwama Kwenye Mpaka wa Slovenia

Maelfu ya wahamiaji wamekwama kwenye mpaka wa kuingia barani ulaya,baada ya mbinu mpya ya kuwadhibiti wahamiaji kutekelezwa.
Watu wengi, wakiwemo watoto wachanga wamekesha nje kwa baridi kali na mvua kwenye eneo lisilomilikiwa na mtu yeyote lililoko katikati mwa Croatia na Slovenia.
Kwa sasa wamepewa hifadhi ya muda karibu na kivukio cha mpakani baada ya shirika la msalaba mwekundu kuingilia kati.
Hali hii imesababishwa na hatua ya Slovenia ya kukataa kuwakubalia wakimbizi zaidi kuvuka mpaka wake na kuingia nchini humo.
Afisa mmoja kutoka chama tawala nchini Slovania, Tanja Fajon anasema juhudi za kutafuta suluhu zinaendelea.
Mabasi yaliyojaa wakimbizi yaliegeshwa mbali na mpaka kusini mwa Serbia ambapo maelfu ya wakimbizi wamezuiliwa na polisi wa kulinda mpaka.
Inasemekana kuwa baadhi yao wamepigana na polisi wanaowazuilia wasiingia nchini humo.
http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/10/151019_migrants_slovenia

Related Posts

Maelfu ya Wahamiaji Wakwama Kwenye Mpaka wa Slovenia
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR