Thursday 9 July 2015

Na hiki ndio Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wakati akihutubia Bunge Mjini Dodoma alichokisema July9,2015

Siku ya leo Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete  amelihutubia Bunge, pia ndio siku ambayo amelivunja Bunge. katika hotuba yake aliofanya bungeni mjini Dodoma alisema ya fuatayo,

Na haya ndio aliyosema wakati akihotubia Bunge: kwa kunukuu alichokisema na ni baaadhi tu yaalivyosema -;
 
'Mwanzoni mwa 2006 kulikuwa na matukio mengi ya ujambazi, niliahidi kwamba hatutawaacha.. Hali imedhibitiwa'.
'Natoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa wanayofanya'
'Jambo ambalo hatujafanikiwa ni tatizo la ajali za barabarani, nalo tunalitafutia mwarobaini'
'Habari kubwa kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu, watu zaidi ya Mil. 11 wameandikishwa kati ya watu Mil.23'
'Naamini kila mwenye sifa ya kuandikishwa na kupigakura atapata nafasi hiyo, labda aamue kukataa mwenyewe'.
'TZ kuna jumla ya Magazeti 16, ya Serikali ni mawili.. Hakuna Uhuru wa Habari?'
'Kuna Radio 115, radio ya Serikali ni moja.. TV zaidi ya 20, TV ya Serikali ni moja.. Hakuna uhuru wa Habari?.
'Sheria ya Vyombo vya Habari ilitungwa lakini haikufanikiwa kupitishwa, tunaachia Bunge lijalo lije kumalizia kazi'.
tumeboresha hali ya hali za wafanyakazi kwa kuongeza kima cha chini cha mshahara toka TZS65,000 mwaka 2006 hadi tzs 300,000 mwaka huu.
tumeongeza idadi ya Majaji lengo nikuongeza nguvu kazi . mahakama  kuu  Majaji wakiume 37 mpaka 89 na Majaji wa kike wameongezeka kutoka 8 hadi 37.
Tumepiga hatua katika haki za wanawake ,wabunge wanawake toka 62 na saa wamefikia 127 pia katika vyuo vikuu saa vimeongezeka kufikia 26 had 52 na wanawake wameongezeka toka 10,000+ hadi kufikia 78,000+
Tumewwza kutenganisha Kazi ya upelelezi na kazi ya kuendesha mashtaka.
Nimeamua kuanzisha Mkoa mpya wa Songwe kwa kuugawa mkoa a Mbeya na kuanzisha Wilaya Mpya 6 ambazo ni Kigamboni,
Pato la Taifa letu limekuwa kwa wastani  7% na sisi ni miongoni mwa mataifa 20 duniani yenye uchumi unao kuwa kwa kasi Zaidi.'IMF wanasema pato la Mtanzania ni kubwa kuliko inavyosemwa, tumebakiza kidogo kufikia pato la kati'.
Ukuaji wa uwekezaji nchini umeongeza mapato ya serikali.
tumeongeza bajeti ya kilimo
Matumizi ya majembe  yamepungua kutoka asilimia 76 hadi 32
Uzalishaji wa wa mazao ya asili umeongezeka, pia uzalishaji wa matunda umeongezeka na hata ule wa maua
tumeweza kujenga mahabara inayoweza kugundua virusi vya Ebola.
Maambukizi ya Maleria yamepunguakwa asilimia 51 na maambukizi  ya ukimwi kutoka 7.1% mpaka 5.5%. 
pia vijiji 5336 Zaidi sasa vimepatiwa umeme kwa mpango wa REA.Na leo 2015 watanzania 40% wanapata umeme toka 10% mwaka 2006.
'Hatujaweza kulifufua Shirika la Ndege, tuko kwenye mpango kuamua jinsi ambavyo tunaweza kulifufua Shirika hilo'.
Tumeongeza bajeti ya barabara toka bilioni 73 hadi  bilioni 800. na tunampango wa kufufua barabara za juu (flyover)za Tazara na Ubungo na kufufua Reli jijijni Dar es salaam
tumeboresha huduma ya afya na uwiano wa wananchi kwa daktari na manesi umeimarika kwa sasa. pia umri wa kuishi umeongezeka toka miaka 49 mpaka 62
Niliahidi kukuza michezo  nimetimiza. soka bado hatujfanyi vizuri, na nimerudisha michezo mashuleni kama njia ya kukuza vipaji kama njia ya kukuza vipaji mbeleni.
'Niliahidi kukuza Michezo na sanaa, kwenye Michezo Serikali imelipia Makocha kwenye kila mchezo'.
Tumekuza na kusapoti Sanaa za aina zote. wasanii wa muziki tumelipa mastering sudio na tumetunga sheria za kulinda haki za wasanii.
'Mwaka 2014 niligharimia Timu ya wazoefu kutoka Marekani kuja kutoa mafunzo kwa wasanii wa Muziki na Filamu','Tukipata maumivu kwenye soka, muziki na movie vinatuliwaza..Wasanii wa muziki na movie wanafanya kazi nzuri kuitangaza TZ'
tumefanya mengi tangu toka nilipoingia madarakani lakini hatujamaliza yote. tumetekeleza 88% ya ilani ya chama na ahadi za serikali.
nilipo safari kwenda nje niliulizwa na mmoja wa wahandishi wa habari kwamba' ungependa watanzania wakukumbuke kwa lipi? Ningependa mnikumbuke kwamba niliwakuta kule  na nawaacah juu Zaidi kimaendeleo.
'Tulipo sasahivi ni bora zaidi kuliko tulipokuwa jana, 'Kinachonipa faraja ni kwamba na mimi nimefanya kitu kwenye kuchangia kukua kwa nchi yetu'.
nawatakia kila jema wabunge wanaorudi  kutetea  nafasi zao majimboni na wakati mwema kwa wale wanaostaafu.
wabunge mliotangaza nia ya urais kunipokea kijiti nawatakia kila la kheri. mpo wengi ipo kazi kubwa kubakiza majina matano tu.Msitununie.
Nashukuru makamu wa Rais mawaziri wakuu wa vipindi vyoteRais w Zanzibar, Makatibu Wakuu viongozi na wenginewote kwa utumishi wao.
'Napenda kumshukuru Mizengo PINDA kwa mchango wake, wakati mwingine alibeba lawama zisizo zake'.
'Namshukuru pia Edward LOWASSA alifanya kazi nzuri wakati wa Uongozi wake kama Waziri Mkuu'.
Namaliza uongozi wamngu nikiwa na wapenda. Nitawamiss kama mtumishi na kama kiongozi wenu.
Nakishukuru chama chetu CCM  kwa kuniamini, naishukuru familia yangu haswa mke wangu kwa kusimama name katika kutekeleza wajibu wangu.
Nawatakia kila la heri katika matamanio yenu ila mko wengi na vigogo wengi
Natangaza kuvunja Bunge Rasmi lakini litaendelea kuwa hai mpaka septemba20, 2015.
 
 
Na hiy ndio hotuba ya ya Mh.Rais wakati akihutubia bunge july9,2015 .....na ni baadhi tu ya vile alivyosema bungeni. kwa stori nyingine Zaidi ungana name facebook, twitter na gmail.com

Related Posts

Na hiki ndio Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wakati akihutubia Bunge Mjini Dodoma alichokisema July9,2015
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR