Thursday 9 July 2015

Dimond Platnumz pamoja na Shilole waguswa na Hotuba ya Mh. Rais

Baada ya Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhutubia Bunge na kuvunja pia rasmi. masanii wa bongo flava Dimond  alizungumza na amplifaya ya clouds fm akisema kwamba;

DIMOND PLATNUMZ;
Kipindi ambacho nimebahatika kumuona Mheshimiwa madaraka na vitu ambacho amevifanya kiukweli ni vitu ambavyo vinagusa sana hususa katika tasnia ya kwetu ya muziki unajua hatujawahi kupata mheshimiwa ambaye akawa anatizama suala la muziki na kulithamini kama la kwake kabisa sio tu suala la muziki na vitu vingi sana mimi sio mtu wa kusikiliza masuala ya siasa wala kuangalia masuala ya kisiasa
 
pia aliendelea kusema;
Leo kwa Mara ya kwanza nilikuwa naendesha gari huku nasikiliza vitu mwanzo mpaka mwisho kuna vitu ambacho alikuwa anazungumza vinagusa moyoni kabisa kuna vitu alikuwa anaongea vya kuchekesha lakini kuna time nilikuwa nafikiri Je rais atakaekuja atakuaje atakuwa kweli anakumbuka jamii yake ukizungumzia kama wasanii na watu wengine kama alivyokuwa anafanya yeye kwasababu sio kila mtu anachukulia suala la sanaa kama serious mwingine anaweza akaona vijana hawa wanaimba imba tu lakini wengine ndio ajira yetu tunafamilia wazazi wetu ndugu marafiki na tumeajiriana wenye kwa wenye kupitia sanaa’
 
amesema pia;
‘Nikajikuta ghafla daah Je Rais atakayekuja ikiwa Je anapenda uvuvi akiwa anapenda vitu vingine labda muziki akaudharua itabidi tukashika nyavu tukavue na suala la muziki linaishia hapo hapo hakuna masuala ya Channel O au MTV nikajikuta nawaza nikajikuta naandika kutoka moyoni hakika katutoa kule anatuacha hapa ambako pako juu zaidi kama kauli yake mwenye alivyosema inagusa moyoni yaani unatamani kama inawezekana wala apewa muhula mwingine aendele tena lakini ndio haiwezekani kisheria lakini ndo hivyo namshukuru sana nampongeza kwa kipindi ambacho akiwa akilihutubia taifa la Tanzania’
 
 
Nae Shilole alizungumza kwenye mtandao wa instagram akisema kwambaa ;
"wasanii wanatupa heshima ,wanatupunguzia hasira za soka"
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

kupata stori Zaidi ya hizi  kutana nami katika facebook, twitter na gmail kwa maoni , na chochote kile.

Related Posts

Dimond Platnumz pamoja na Shilole waguswa na Hotuba ya Mh. Rais
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR