Friday, 19 June 2015

GOLDEN STATE WORRIORS KUTWAA TAJI KATIKA FINALI YA MWISHO DHIDI YA CLEVELAND CAVALIERS


 Golden State Warriors watwaa taji katika ligi kuu ya nbaa huko marekani katika mchezo wa mwisho dhidi ya cleveland, kwa kuifunga vikapu 105-97. katika finali hiyo Stephen curry pamoja na Andre Iguodala  walikua ndio wachezaji bora katika mchezo huo (MVP).
Stephen Curry akiwa na point 25 huku mpinzani wake James akiwa na point 32. golden warriors wameshinda michezao 4-2 dhidi ya cavaliers.

Steve Karr ambae ni kocha wa kwanza wa golden state warriors alisema anashukuru ya kwamba katika msimu huu mambo yalienda vizuri mpaka kufika finali. Kerr pia alipata pongezi kutoka kwa aliekuwa kocha wa nba Phil Jackson na Gregg Popovich.Ni miaka 40 imepita tangu timu hii kutwaa taji ya NBA.



kwa upande wa Lebron James alisema alisikitishwa na kushindwa kutwaa taji hilo. Cleveland Cavaliers alikuwa na majeruhi wa 2, Kyrie Irving na Kevin Love ambao hawakweza kushiriki kikamilifu katika finali hizo tangu mwanzo.katika maneno yake Lebron James alisema "we run out of talent".

Lebron James dhidi ya mpinzani wake Stephen Carry



                                      BOFYA HAPO CHINI UTAZAME JINSI MECHI ILIVYOKUWA.



Related Posts

GOLDEN STATE WORRIORS KUTWAA TAJI KATIKA FINALI YA MWISHO DHIDI YA CLEVELAND CAVALIERS
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR