Saturday, 12 December 2015

Manchester Unitrd Yapoteza Mchezo Dhidi ya Bournemouth

Bournemouth 2 - 1 Manchester United

Stanislas 2                      Fellaini 24     
King 54
Manchester United ikiwa nyumbani kwa Bournemouth imepoteza mchezo baada ya kupokea kichapo cha mabao 2 - 1. Katika mchezoo huo goli la kwanza lilifungwa na Stanislas katika dakika y 2 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo lakin bao hilo lilirejeshwa na Manchester United katika dakika 24 ya kipindi cha kwanza na bao hilo likifungwa kupitia Fellaini.

Katika kipindi cha Pili cha mchezo huo Bournemouth ilifanikiwa kuongeza bao la pili katika dakika 54 likifungwa kupitia mchezaji wa zamani wa Manchester United Joshua King amabe sasa anachezea timu hiyo ya Bournemouth, Na hivyo kuipa timu hiyo Ushindi hadi mwisho wa mchezo.
Manchester United itashuka hadi nafasi ya tano endapo Tottenham atashinda mchezo wake dhidi ya Newcastle United hapo Jumapili. Kwasasa Bournemouth wanashikilia nafasi ya 14 katika msimao wa ligi ya Uingereza Primier League.
Katika Mchezo huo mchezaji bore alikuwa ni Junior Stanislas akiwa maegusa mpira mara 62 kuliko wachezaji wenzake wa Bournemouth.

Related Posts

Manchester Unitrd Yapoteza Mchezo Dhidi ya Bournemouth
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR