Friday, 12 June 2015

MSANII MYSTORY KUACHIA BONGE LA JOINT.

 Mystory afanya collabo na msanii Chemical pamoja na Yuzo.

   Msanii MYSTORY ameonesha nia sasa ya kuingia kikamilifu katika gemu la muziki na kwa sasa anakuja na ngoma alio mshirikisha rapa wa kike ambae nae ni wa hatari kwa aina yake anajuikana kwa jina la MYSELF a.k.a CHEMICAL ambaye ameachia tayari ngoma yake inayofanya vizuri kila station za radio hapa nchini SIELEWI ndo jina la wimbo wa bi mdada huyo mbali na mwana dada huyo lakini pia Rapa Mystory amemshirikisha jamaa kutoka East coast anaejulikana kwa jina la Yuzo ambae kwa mara ya kwanza ameanza kusikika katika wimbo wa KING CRAZY GK  wa baraka au laana kwa kweli ni bonge moja la joint ambalo naamini litafanya vizuri kibongo bongo.
    Mbali na maisha ya muziki rapper huyo ni mwanachuo wa Chuo kikuu cha Dar es salaam (katika shule kuu ya Uhandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma) hivyo naamini kwa anachokisomea na hiki anachokifanya ni vitu vinavyoendana sawia.
      "Naamini kwamba watu wataipokea vizuri kwani joint na chemistry nzima ya uandaji ilienda poa nimechagua kolabo ambayo ni sahihi kabisa kwani Chemical ni msanii mzuri na Yuzo vile vile" alisema Mystory.
         Hivyo watanzania hatuna cha kufanya zaidi ya kuendelea kusubiri kwani kwa chemistry iliyopo tunaamini kila kitu kitaenda vizuri mungu akuongoze bwana Mystory.

Related Posts

MSANII MYSTORY KUACHIA BONGE LA JOINT.
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR