Thursday, 11 June 2015

JANUARY MAKAMBA PAMOJA NA WANACHAMA WENZAKE WA CCM KUCHUKUA FOMU YA URAIS

January Makamba akichukua fomu ya Urais.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia January Makamba pamoja na wanachama wenzake wa CCM, Eldeforce Bilohe, Willium Ngeleja, Boniface, Dengo, Mathias Chikawe tayari wamesha chukua fomu za kuwania Urais mjini Dodoma, kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) baada ya kutangaza nia. Makamba alisema anaamini CCM itakwenda kuchagua kiongozi bora ambaye atakwenda kuwania nafasi hiyo ya Urais.


Makamba akiwa anazungumza na vyombo vya habari mjini dodoma alisema haingi katika kuwania nafasi hiyo kwa ajili ya kujaribu ama kujipanga kwa uchaguzi ujao. 
Mimi ndio nina nafasi kubwa kushinda kwenye uchaguzi mkuu ujao nina uwezo , maaarifa, ukomavu, na dhamira thabiti, alisema Makamba mjini Dodoma akizungumza na vyombo vya habari nchini.
kamati ya uchaguzi CCM ilisema mpaka sasa January Makamba anaongoza kwakuwa na wadhamini wengi kuliko wagombea wengine ambao wameshakwisha kuchukua fomu wa Chama cha Mapinduzi, ambapo mjini Dodoma alidhaminiwa na wanachama 1,200 wa CCM. na sasa anazunguka kwenda mikoa mingine ilikupata wadhamini wengine. kwakumaliza alisema akipata nafasi hiyo ataenda mbele zaidi ya alipoishia Rais Jakaya Kikwete.
Nae Mkulima Eldeforce Bilohe ambaye nae alichukua fomu ya Urais  bila ya kuwa na fedha ya kuchukulia fomu kiasi cha shilingi millioni moja hapo jana naye alisema mpaka sasa hajaona mwanachama aliye mwona ni tishio kwake kati ya wagombe 27 ambao wameshakisha kuchukua fomu za Urais.
matiasi chikawe ambae alichukua fomu ya Urais hapo jana mjini Dodoma.
Eldeforce Bilohe ambaye aliyeshindwa kuchukua fomu kwakutokua na fedha za fomu ya Urais.


Related Posts

JANUARY MAKAMBA PAMOJA NA WANACHAMA WENZAKE WA CCM KUCHUKUA FOMU YA URAIS
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR