Saturday, 13 June 2015

ALI KIBA AONGOZA KWA USHINDI WA TUZO 5 ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS(KTMA)

Katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards(KTMA)zilizo fanyika hapo jana, Msanii maarufu Ali kiba alingoza kwa kuchukua tuzo 5 ,katika kategori sita alizo shindanishwa. Ambazo ni Wimbo bora  wa Afro Pop, Mtunzi bora wa bongo Flava,  wimbo bora wa mwaka,  mwimbaji bora wa kiume wa bongo fleva na Mtumbuizaji bora wa kiume.
Dimond Platnumz alishinda tuzo 2 ambazo ni video bora ya mwaka, na wimbo bora una sikilizwa Zaidi.
Mzee Yusufu akipata tuzo 2 ambazo ni mwimbaji bora wa kiume katika taarabu na mtunzi bora wa taarabu.
Joh Makini nae alipata tuzo 2 : Mtunzi bora wa nyimbo za hip hop na msanii bora wa mwaka wa hip hop.
Vanessa Mdee alishinda tuzo 2: Mtumbizaji bora   wa muziki wa kike na mwimbaji bora wa kike wa bongo fleva.
Isha Mashaiuzi hakua nyuma nae alishinda tuzo 2: Wimbo bora wa mwaka wa taarabu na  mwimbaji bora wa kike wa taarabu.
Jose Mara nae alishinda tuzo 2: Mwimbaji bora wa kiume katika bendi na Mtunzi bora wa nyimbo kwa upande wa bendi. 
Profesa J. alishinda tuzo 1 ya wimbo bora wa hip hop, pamoja na NahReel ambaye alishinda tuzo1: Mtayarishaji bora wa bongo fleva. 
Jux  alishinda tuzo 1  : wimbo bora wa mwaka RNB
Baraka Da Prince alinyakua tuzo 1: msanii bora chipukizi,
Mrisho Mpoto alishinda tuzo 1: wimbo bora wenye vionjo vya asili ya kitanzania.
Enrico nae slishinda tuzo 1: Mtayarishaji bora wa nyimbo za taarabu.
Ferguson alishinda tuzo 1 kama rapa bora  katika bendi.
Amiroso nae tuzo 1:  mtayarishaji bora wa mwaka
Yamoto band nao walishinda tuzo 1: kundi bora la mwaka,
Jahazi modern teerabu walishinda tuzo 1: kundi bora kwa upande wa taarabu wakiwakilishwa na Mzee Yusufu ,
Fm academia nao tuzo 1: bendi bora ya mwaka
Kolabo bora ya mwaka ilienda kwa Mwana Fa na Ali kiba
Wimbo bora wa Kiswahili kwa upande wa bendi tuzo ilikwenda kwa: bendi ya Vijana wa Ngwasuma
Tuzo nyingine zilikua, pia tuzo ya wimbo bora wa Africa Mashariki ilikwenda kwa kundi la Sauti Solo, 
Tuzo ya wimbo bora wa rege /dance hall ilikwenda kwa  Maua Sama.



Related Posts

ALI KIBA AONGOZA KWA USHINDI WA TUZO 5 ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS(KTMA)
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR