Saturday, 25 June 2016

RONALDO ASHINDWA KUVUNJA REKODI ULAYA

Jumapili,26 June 2016



Nyota wa timu ya taifa ya Ureno na Real madrid akikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora Ulaya  na aliyekua raisi wa shirikisho la soka Ulaya,Michel Platini.

Mshambuliaji Nyota wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid,hii leo ameshindwa kuandika rekodi mpya ya ufungaji bora wa muda wote wa michuano ya mataifa ya Ulaya(Euro) baada ya kutofunga katika mchezo wa timu yake ya taifa dhidi ya Croatia katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Mchezaji huyo ghali zaidi duniani alikua ana nafasi nzuri ya kuifikia rekodi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na mchezaji na nahodha wa zamani  wa timu ya taifa ya Ufaransa Michel Platini ambae  pia alikua raisi  wa shirikisho la soka barani Ulaya,Uefa.

Michel Platini akishangilia baada ya kufunga goli katika moja ya mechi zake za michuano ya Ulaya Euro alipokua akiichezea Ufaransa.

Platini ambae pia amewahi kuzichezea klabu za Nancy,St.Etiene na Juventus, anaongoza orodha ya wafungaji wa michuano hiyo akiwa na magoli Tisa(9) aliyofunga katika jumla ya michezo mitano huku Ronaldo  akifuatia baada ya kucheza michezo 18 ya michuano hiyo huku akifunga magoli nane (8) pekee.

  
Michel Platini (kushoto) akiwa na beji ya unahodha wa timu ya Taifa ya Ufaransa mkononi,kama ilivyo kwa Christiano Ronaldo (kulia) na timu ya taifa ya Ureno.

Pia katika orodha hiyo wapo nyota wengine kama Alan Shearer mwenye  magoli saba(7),Pia Thiery Henry na Zlatan Ibrahimovich wenye magoli sita (6) kila mmoja.
Lakini pia Nyota wengine ambao wapo  kwenye orodha hiyo na bado wanashiriki michuano hiyo mpaka sasa ni Wayne Rooney wa Uingereza na wajerumani wawili,Lukas Podolski na Mario Gomez waliofunga magoli manne (4) kila mmoja lakini pia Gareth Bale wa Wales ambae amefunga magoli matatu na hivyo wote kuwa katika nafasi nzuri  ya kuweza kuifikia rekodi hiyo.




Habari na Mzigu Petro

Related Posts

RONALDO ASHINDWA KUVUNJA REKODI ULAYA
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR