Mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala imeiamuru kampuni ya mawasiliano Tigo Tanzania kuwalipa fidia wanamziki wa bongo fleva, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA pamoja Ambwene Yesaya aka AY jumla ya kiasi cha Sh.2.18 Bilioni za kitanzania. Kwa kosa la kutumia nyimbo yao kama Caller tune( mwitikio wa simu) bila ruhusa na mkataba.
Taarifa kutoka The Citizen zinasema;
Kampuni hiyo ilikuwa imepeleka pingamizi la hukumu hiyo ya mahamaka ya hakimu mkazi Ilala katika mahakama kuu ya Tanzania. Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Jumanne hii lakini imeahirishwa hadi Ijumaa.
Madai ya Mwana FA na AY ni kuwa Tigo ilitumia kazi zao bila kuwa na mkataba nao wowote au kampuni ya kati iliyowawakilisha na hivyo kuingiza fedha ambayo wawili hao wanaamini ni nyingi.
Awali walitaka walipwe fidia ya shilingi bilioni 4.3.

Mwana FA. AY Walipwa Fidia...
4/
5
Oleh
kwetutz24