Friday 26 February 2016

Gianni Infantino Awa Rais Mpya wa FIFA

Shrikisho la Soka Duniani FIFA limefanya uchaguzi hivi leo Feb 26, 2016 wa kumchagua Rais mpya wa FIFA atakae chukua nafasi ya Sepp Blatter aliyeongoza shirikisho hilo kwa miaka 18.
Katika Uchaguzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shrikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) kwa miaka saba, Gianni Infantino alinyakuwa nafasi hiyo ya Urais.
Gianni Infantino alishinda mzunguko wa pili kwa kura 115 dhidi ya mpinzani wake Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa kura 88 ambae walipishana nae kwa kura 27. huku akifuatiwa na Prince Ali bin al-Hussein aliye pata kura 4  na watatu akiwa Jerome Champagne ambae hakupata kura yoyote.
  • Gianni Infantino - 115 votes
  • Sheikh Salman - 88 votes
  • Prince Ali al-Hussein - 4
  • Jerome Champagne - 0
Rais huyo mwenye umri miak 45, ameihaidi kurejesha mpira FIFA.
“bring football back to Fifa" alisema.
Infantino atakuwa Rais wa tisa kushika nafasi hiyo, baada ya Blutter kushika nafasi hiyo kwa mihula mitano  kuanzia mwaka 1998 kabla ya kujiuzulu mwishoni mwa mwaka jana na kufungiwa miaka 6 kutojihusisha na soka kutokana na tuhuma za kuvunja taratibu na kanuni za FIFA.

Related Posts

Gianni Infantino Awa Rais Mpya wa FIFA
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR