Friday 30 October 2015

Dr. John Pombe Magufuli Amemekabidhiwa Cheti cha Ushindi na Mwenyeketi wa Tume ya Uchaguzi NEC..

Baada ya Uchaguzi Mkuu Kukamilika nchini Tanzania tume ya uchaguzi NEC chini ya kiongozi wao Damian Lubuva Dr. Magufuli alitangazwa rasmi kama Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alishinda kwa kura 8,80935 ikiwa sawa na asilimia 58.47.
Siku ya Leo rais huyo mteule Dr. Magufuli  akiwa pamoja na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan ambe ndie atakae kuwa makamu wa rais wamelikabidhiwa rasmi vyeti vya ushindi na Jaji Mastaafu Damian Lubuva ambae ni mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi NEC baada ya kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oct.25.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi wa Damond Jubelee ulioko eneo la Upanga jijini Dar es Salaam. Na baaada ya kukabidhiwa vyeti hivyo walielekea kaitika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi ilioko eneo la lumumba.


Tume ya uchaguzi NEC ilimtangaza Dr. Magufuli kama mshindi wa Uchaguzi mkuu uliofanyika hapo Jumapili ambapo alishinda kwa kura 8.882,935  ikiwa sawa na asilimia 58.46.
Huku mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa akishinda kwa kura 6,072,848 ikiwa sawa na asilimia 39.97.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Mh.Edward Lowassa alipinga matokeo hayo na hakukubaliana na nayo na kusema kuwa ameibiwa kura na kwamba yeye ndiye mshindi katika uchaguzi huo.

Related Posts

Dr. John Pombe Magufuli Amemekabidhiwa Cheti cha Ushindi na Mwenyeketi wa Tume ya Uchaguzi NEC..
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR