Saturday, 1 August 2015

Mtoto mwenye Miezi 18 achomwa moto mpaka kufa na familia nne kujeruhiwa huko Palestina









Mtoto wa kipalestina amechomwa mpaka kufa na familia nne kujeruhiwa katika shambulizi la uchomaji na wanaodhaniwa kuwa ni walowezi wa kiyahudi katika nyumba mbili  zilizopo katika ukingo wa Magharibi siku ya ijumaa.



Waziri Mkuu wa Palestina Benjamini Netanyahu alikiita kitendo hicho cha kulipua  kijiji cha Duma karibu na kaskazini mwa mji wa Nablus kuwa ni "kitendo cha kigaidi katika kila heshima' na kutoa amri kwa vikosi vya ulinzi kuwatafuta wahusika..


Mashambulizi hayo yamezidi kuleta mvutano kati ya Israil na Palestina, siku mbili baada ya Netanyahu kuthibitisha kuwepo kwa nyumba mpya 300 za walowezi katika Ukingo wa Magharibi.

Shirika la ukombozi la Palestina limesema kuwa serikali ya Netanyahu inahusika na kifo cha mtoto huyo mwenye miezi 18 Ali Saad Dawabsha, likizungumza kuwa tukio hilo linakwenda sambamba na miongo  ya ukatili iliyotolewa na serikali ya israeli kwa walowezi wa kigaidi.
Rais wa Palestina Mahmud Abbas  ameitwa kwa ajili ya uchunguzi na Mahakama ya Kimataifa huko The Hague


kwa mujibu wa maafisa ulinzi wa palestina, wanasema kuwa washambulihaji hao wanne wanaaminika kuwa ni walowezi wa kiyahudi waliwasha nyumba moto katika malango ya kijiji hicho na kuchora michoro ukutani kabla ya kukimbilia karibu na makazi ya kiyahudi.


Majeshi ya israeli na jeshi la radio limesema nyumba mbili zilichomwa moto na watu wawili waliojifunika nyuso zao na kuua mtoto na kujeruhi familia nne . wakiongeza kuwa michoro hiyo iliandikwa kwa kiebrania. vyanzo vya habari vya palestina vilisema majeruhi wamepelekwa hospitali.
 
taarifa toka hospitali zinaesema mtu awa nne aliyejeruhiwa hakuweza kujulikana mapema. na baada ya hapo, vyombo vya habari vilitoa taarifa kuwa mchoro ule ulikuwa unamaanisha  "kisasi" na "aishi milele Mesia" na kwamba washambuliaji walirusha mabomu ndani ya nyumba hizo mbili, ambapo moja ilikuwa hainakitu.
waziri wa ulinzi wa israeli Moshe Yaalon amesema shambulizi kama hilo  halitaendelea kuvumiliwa na kuongeza kuwa " hatuta endelea ruhusu magaidi kuchukua maisha ya wapalestina"

majeshi ya Israeli yamesema bado yanafanya kazi ya kuwatafuta  wahusika.

Related Posts

Mtoto mwenye Miezi 18 achomwa moto mpaka kufa na familia nne kujeruhiwa huko Palestina
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR