Sunday, 9 August 2015

Mourinho atupia lawama kwa madaktari wa timu yake, baada ya kutoka sare na Swansea.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekosoa madaktari wa timu yake kwa kumfanyia matibabu Eden Hazard katika mechi waliyo toka sare na Swansea.alisema kuwa hakufurahishwa na daktari Eva Carneiro kuingia uwanjani na kumtibu Hazard.


Goli kipa wa chelsea Thibaut Courtois aliolewa nje kwa kulimwa kadi nyekundu, na kuipa Swansea penati ambapo mchezaji wa swansea Bafetimbi Gomis alishinda na kuwafanya wawe sare ya bao 2-2.
Na kufanya timu hiyo kubakiwa na wachezaji tisa uwanjani, baada ya Eden kutolewa nje ya uwanja kwa matibabu zaidi. japo kwa Mourinho yeye aliona hakuwa na maumivu makubwa.

Mourinho aliviambia vyombo vya habari kuwa, Kama mchezaji akipata matibabu wanapaswa watoke nje ya uwanja.
alisema pia,
 "siku furahia kitendo walichofanya madaktari wangu.walikuwa hawajitambui na wasiojua kitu. Hata kama ni daktari ama katibu katikia benchi unatakiwa kufahamu mchezo. unatakiwak ufahamu kuwa unapungufu ya mchezaji mmoja na ili kumsaidia mchezaji ni lazima uwe na uhakika na tatizo alilonalo. Nauhakika Eden hakuwa na tatizo kubwa. alikuwa amejigonga tu,na alikuwa amechoka".
 

Related Posts

Mourinho atupia lawama kwa madaktari wa timu yake, baada ya kutoka sare na Swansea.
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR