Monday 29 June 2015

WATU 30 KUTOKA UINGEREZA WARIPOTIWA KUUWAWA KATIKA SHAMBULIZI LILIOFANYIKA TUNISIA

 








 
Ni siku chache tu zimepita tangu kufanyika kwa shambulizi la kigaidi nchini Tunisia anailiripotiwa kuwa katika shambulizi hilo watu 39 waliuawa.
na baada ya hapo operesheni ya kusaka watuhumiwa wa shambulizi hilo walitafutwa.
lakini baada ya kufanya utafiti imegunduliwa kuwa watu 30 kutoka Uingereza kati ya wale 39 waliuawa katika shambulizi hilo ambalo lilifanywa na Seifeddine Rezgui ambae aligundulika kwamba ndie alikuwa ufukweni kabla ya kufanya shambulizi hilo. 
Baba mzazi wa Seifedden Rezgui alisema ameshitushwa na kitendo hicho cha mwanae, kwakuwa anajua mwanae hajawai kuhusika na vitendo kama ivyo na aliomba radhi kwa tukio hilo.

Sasa uchunguzi wa kina unafanyika tokea eneo la tukio la SOUSSE ambako ndiko shambulizi lilikoanzia, na zaidi ya maafisa polisi na wafanyakazi toka Uingereza nao wamejumuika katika uchunguzi huo.

wananchi wa tunisia wameonywa kuwa makini kwasababu inawezekana mashambulizi bado yakaendelea katika mji huo. japo kuwa ulinzi kwa sasa umeimarishwa nchini Tunisia.
pia taarifa zinasema kwamba wathirika wa shambulio hilo ni watu wa vizazi vitatu wa familia moja.


waingerza wakiaga miili ya marehemu wealiofariki katika shumbulizi huko Tunisia.





Related Posts

WATU 30 KUTOKA UINGEREZA WARIPOTIWA KUUWAWA KATIKA SHAMBULIZI LILIOFANYIKA TUNISIA
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR