Friday 14 August 2015

Wanafunzi saba wamezama katika bahari ya India nchini katika ufukwe wa Dian, Kenya

Wanafunzi saba kutoka shule ya msingi ya St.Martin De Pores Boys wamefariki dunia baada ya kuzama katika ufukwe wa Dian nchini Kenya.


wanafunzi hao walikua wakiogelea katika ufukwe wa Bidi Badu wakati mawimbi mepesi yalipo panda kwa gafla na kuwa makali na katika bahari na kuwazamisha watoto hao.

kulingana na taarifa za msalaba mwekundu nchini Kenya, wanafunzi 52 kutoka shule ya Muranga waliokolewakatika bichi ya Pavilion, Diani, katika kata ya Kwale wakati wanafunzi wengine wanne wakipelekwa hospitali.

Waokoaji na wafanyakazi wa msalaba mwekundu nchini humo walifanya juhudi kubwa ya kuitafuata miili hiyo ya wanafunzi wakati wa usiku.
Wanafunzi hao  56 walikua katika safari ya kutembelea ufukwe wa Dian. wanafunzi hao walibebwa na mawimbi makali yaliyowasomba na kuwatupia mbali wakati wakiogelea katika ufukwe wa Pavilion.

Baada ya miili hiyo kupatikana,Miili ya wanafunzi hao ililazwa katika mochwari iliyoko katika hospitali ya Pandya ikisubiriwa iliitambuliwe na wazazi wao.
Tukio hilo limetokea miezi michache tu iliopita  baada wanafunzi wanne kutoka shule ya shimba hills huko Kwake kuzama katika bichi hiyo hiyo baada ya kusombwa na mawimbi makali wakati wakiogelea.


Related Posts

Wanafunzi saba wamezama katika bahari ya India nchini katika ufukwe wa Dian, Kenya
4/ 5
Oleh
Show Comments: OR