Mfululizo wa milipuko katika Ghala huko Kaskazini mwa Bandari ya mji wa China na kuuwa watu 17, na idadi ikiendelea kuongezeka , mashuhuda wamesema kuwa moto ulikuwa ukionekana unalipuka angani katika usiku huo.
ripoti kutoka shirika la habari China limeongeza kuwa, wafanyakazi wa kikosi cha kuzima moto 12 wamefariki wakati wakifanya juhudi za kuuzima moto huo.
Waandishi wa Shirika la habari la AFP wamesema kuwa walishuhudia milio ya vioo vya magari vikipasuka kilometa 13 kutoka eneo walilokuwa.
mmoja wa mashuhuda wa moto huo ambae nyumba yake ilikuwa karibu na bandari hiyo ambapo tukio hilo lilitokea amesema kuwa, moto huo ulikuwa mkubwa , na inadhaniwa kuwa ulikuwa mkubwa kiasi cha mita 100 kwa urefu.
Nilisikia mlipuko wa kwanza na kila mmoja alitoka nje, na baada ya hapo kukawa na mfululizo wa milipuko, madirisha yalivunjika na watu wengi walio kuwa ndani waliumia na kutoka nje huku wakikimbia huku wakiwa na damu.
watu 17 waliuwawa na zaidi ya 400 kupelekwa hospitali. Rais wa China Xi Jinpin kupitia mtandao wa twitter alisema watu wote watoke nje na kwenda kuwaokoa wahanga na wakazime mto.
shirika la habari la nchini china Xinhua limethibitisha kuwa idadi ya majeruhi imezidi kuongezeka na kufikia 32.
IDADI YA VIFO KATIKA MLIPUKO WA MOTO HUKO TIANJIN - CHINA
4/
5
Oleh
kwetutz24