Rais Magufuli hivi leo amemalizia uteuzi wake wa mawaziri na manaibu wake amabo hakuwamalizia pindi alipotangaza baraza jipya la kwanza la Mawaziri katika awamu yake ya Tano.
Uteuzi
1. Professa Jumanne Maghembe - Waziri wa Maliasili na Utalii
2. Dkt. Philip Mpango - Waziri wa Fedha na Mipango 9ni baada ya kteuliwa kuwa Mbunge)
3. Mhandisi Gerson Lwenge - Waziri wa Maji na Umwagiliaji
4. Dkt. Joyce Naelichako - Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia, na Ufundi (ni baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge)
5, Mh. Hamad Masauni - Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
6. Prof. Makame Mbarawa - Amehamishwa kutoka Wizara ya Naji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri
watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na
kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015